1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Mahasimu wa Sudan wakutana tena kujadili suluhu ya mzozo

30 Oktoba 2023

Majenerali hasimu wa Sudan Mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan na makamu wake wa zamani Mohamed Hamdan Daglo, anaeongoza Kikosi cha wanamgambo (RSF) wamekutana Saudi Arabia kujadili hatma ya mzozo unaoendelea Sudan.

https://p.dw.com/p/4YCLE
Majenerali wa jeshi Sudan Abdel Fattah al-Burhan na Mohamed Hamdan Daglo
Majenerali wa jeshi Sudan Abdel Fattah al-Burhan na Mohamed Hamdan Daglo Picha: Mahmoud Hjaj/AA/picture alliance

Mazungumzo yalianza alhamisi wiki iliyopita mjini Jeddah huko Saudi Arabia na ndani ya Sudan inaelezwa kwamba hakuna dalili  za kumalizika kwa haraka mapiganao yanayoendelea.

Katika muda wa miezi sita, vita kati ya majenerali hao hasimu yamesababisha mauaji ya zaidi ya watu 9,000 na wengine karibu milioni sita wamekimbia.

Soma zaidi: Jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF wako tayari kushiriki mazungumzo Jeddah

Huko Khartoum, ambapo jeshi la wanahewa limeshindwa kuwaondoa wanamgambo wa RSF, ambao wanadhibiti mitaa ya mji mkuu huku jeshi likishikilia eneo la Mashariki mwa nchi hiyo.

Wakati mazungumzo yalipoanza, RSF ilidai kuwa imeteka nyara, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kusini na jiji kubwa zaidi katika eneo la magharibi la ambayo ni ngome ya jadi ya RSF.

Mazungumzo hayo ya amani ya Jeddah  yanalenga kupata suluhu ya kusitisha mapigano na kufungua njia ya kuwasilishwa misaada ya kibinadamu nchini Sudan.

Jenerali Mkuu wa jeshi wa Sudan Abdel Fattah al-Burhan
Jenerali Mkuu wa jeshi wa Sudan Abdel Fattah al-BurhanPicha: Craig Ruttle/AP/picture alliance

Kwa mujibu wa taarifa kutoka wizara ya mambo ya nje ya na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani 'mazungumzo hayatashughulikia masuala mapana ya kisiasa'.

Akizungumza kwa sharti la kutokutajwa jina, afisa wa zamani wa jeshi aliliambia Shirika la habari la Ufaransa AFP, Kikosi cha  RSF kitaimarisha udhibiti wake katika jimbo laDarfur.

Soma zaidi: Marekani yatiwa wasiwasi na mashambulizi ya RSF

Mauaji ya kikabila yaliyochochewa na RSF na wanamgambo washirika yalisababisha uchunguzi mpya unaofanywa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu.

Nyala, mji ambao ni kitovu cha kiuchumi cha jimbo hilo ni kituo kikubwa zaidi cha kijeshi katika majimbo matatu ya , Darfur ya Kati na Darfur Mashariki'.

Mahakama ya ICC inachunguza uhalifu wa kivita Sudan.

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivitaICC tangu miaka ya 2000 imekuwa ikichunguza uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya binadamu na mauaji ya halaiki huko Darfur, yaliyofanywa na wanamgambo wa

Wakaazi wa kitongoji cha Al-Wadi wamesema, ''wapiganaji wa RSF wameenea katika jiji lote na wameeleza kuwa hawajaona jeshi tangu siku ya Jumatano. Lakini  jeshi lilijibu kwamba kitengo cha 16 kilizuia shambulio lililosababisha hasara kbwa kwa watu na upotevu wa mali zao"
  
Baada ya miezi kadhaa ya mapigano, hatua ya karibuni kabisa ilikuja wiki iliyopita, wakati "wanamgambo wa RSF waliposhambulia  kitengo cha 16 na magari 300 ya kivita.

Kikosi cha wanamgambo cha (RSF)
Kikosi cha wanamgambo cha (RSF)Picha: Ashraf Shazly/AFP

Majaribio ya awali ya Marekani na Saudi ya upatanishi katika vita yakifanikiwa kufikia makubaliano yaliyoheshimiwa  kwa muda mfupi  tu, na baadae kukiukwa.

Wachambuzi wamesema wanaamini jenerali  Burhan na Daglo walikuwa wamechagua badala ya kuendeleza vita na ugomvi, wamehitaji kupata suluhu kwa njia ya makubaliano zaidi katika meza ya mazungumzo.