1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

IRC yatahadharisha kuongezeka machafuko mkoa wa Darfur

5 Julai 2023

Shirika moja la kimataifa la msaada wa kiutu limetahadharisha juu ya kuongezeka kwa machafuko kwenye mkoa wa Darfur uliopo magharibi mwa Sudan.

https://p.dw.com/p/4TShk
Sudan Khartoum
Vita vya SudanPicha: Stringer/IMAGESLIVE via ZUMA Press Wire/picture alliance

Shirika moja la kimataifa la msaada wa kiutu limetahadharisha juu ya kuongezeka kwa machafuko kwenye mkoa wa Darfur uliopo magharibi mwa Sudan ambao unaandamwa na ukosefu wa usalama kwa miaka kadhaa.

Shirika hilo la International Rescue Commitee (IRC) limesema ndani ya muda wa wiki mbili zilizopita, karibu watu 36,000 wameukimbia mkoa huo na kuingia taifa jirani la Chad kutokana na kutanuka na ghasia za kikabila.

Mkuu wa huduma za dharura za shirika la IRC nchini Sudan Mwiti Mungania amesema hali hiyo imezidisha wasiwasi wa kuongezeka kwa idadi ya wakimbizi katika taifa ambalo tayari linakabiliwa na mzozo.

Hadi sasa jumla ya watu 190,000 wamelikimbia eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo na wale waliouhama mkoa wa Darfur wanasema wamefanya hivyo kuepuka machafuko. Machafuko yameongezeka nchini Sudan tangu kuanza kwa uhasama kati ya majenerali wawili wanaowania madaraka mnamo mwezi April na hadi sasa juhudi za kusitisha mapigano hazijafanikiwa.