1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Burhan ajitokeza hadharani miezi 4 tangu vita vianze

25 Agosti 2023

Mtawala wa kijeshi wa Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, anatembelea kambi za jeshi nje ya mji mkuu, Khartoum ikiwa ziara yake ya kwanza nje ya mji huo tangu mapigano yazuke mnamo mwezi Aprili.

https://p.dw.com/p/4VaQZ
Sudan | General Abdel Fattah Al-Burhan
Picha: Sudanese Army/AFP

Kupitia video zilizosambazwa na jeshi la Sudan leo, Burhan ameonekana akiitembelea ghala la silaha la Atbara iliyo katika jimbo la kaskazini la Mto Nile.

Kiongozi huyo wa jeshi ameonekana akibebwa na wanajeshi waliokuwa wanashangilia.

Duru za serikali zinaarifu kwamba Burhan anakusudia pia kufanya ziara nje ya Sudan kwa mazungumzo katika nchi jirani.

Soma zaidi: Jenerali wa juu wa Sudan amshutumu mpinzani wake kwa uhalifu na kuwadanganya raia

Haya yanafanyika wakati ambapo Umoja wa Mataifa umeonya kwamba huenda vita hivyo vikaenea katika eneo zima na kusababisha mzozo wa kiutu.

Jeshi la Sudan limekuwa likipambana na wapiganaji wa RSF kuwania udhibiti wa mji mkuu, Khartoum, na miji kadhaa ya nchi hiyo tangu Aprili 15.