1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ICC yamfutia mashitaka kiongozi wa waasi Afrika ya Kati

Hawa Bihoga
19 Oktoba 2023

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imefutilia mbali mashtaka 20 yakiwemo ya mauaji, unyanyasaji na mateso dhidi ya waziri wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya kukosekana kwa ushahidi na mashahidi waliopo.

https://p.dw.com/p/4Xl5p
Den Haag | Maxime Jeoffroy Eli Mokom Gawaka
Maxime Jeoffroy Eli Mokom GawakaPicha: Piroschka van de Wouw/AP Photo/picture alliance

Katika tamko lake alilolitowa siku ya Alkhamis (Oktoba 19), mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama hiyo, Karim Khan, alisema kwamba anaondowa mashtaka yote dhidi ya Maxime Jeoffroy Eli Mokom Gawaka kwa sababu hakuna tena sababu yoyote ya kuridhisha kuhukumiwa kwake kutokana na mashauri hayo.

Soma zaidi: CAR, makundi 14 ya waasi wafikia makubaliano ya amani

Wakati wa kusikiliza shauri hilo mnamo mwezi Agosti, upande wa utetezi uliwaambia majaji kwamba waendesha mashtaka walikuwa wametoa ushahidi ambao unaweza kumuondolea hatia Mokom hata kabla ya kukamatwa kwake katika taifa jirani la Chad mwaka 2022.

Mokom alishtakiwa kwa kuratibu shughuli za kundi la anti-Balaka ambalo lilipigana dhidi ya kundi jengine la Seleka.

Mapigano hayo yalisababisha maelfu ya watu kuuwawa na wengina kadhaa kuyahama makaazi yao baina ya mwaka 2013 na 2014.