Hatma ya vikosi vya Ufaransa Mali mashakani
13 Februari 2022Mahusiano kati ya Paris na utawala wa kijeshi mjini Bamako yamezorota tangu Ufaransa ilipotangaza kuwaondoa wanajeshi wake kutoka baadhi ya kambi kaskazini mwa koloni lake hilo la zamani zamani, kupunguza idadi ya askari na kujikita kwenye kuwasaka viongozi wa kijihadi katika eneo hilo.
Ukikabiliwa na shinikizo baada ya kukataa kufanya uchaguzi uliopangwa mwaka huu, utawala wa kijeshi umeishutumu Ufaransa kwa usaliti, kuigawa nchi hiyo na upelelezi, na hata kuwataja askari wa nje wa Ufaransa kuwa ni mamluki. Wakati wote huo utawala wa Mali ulikuwa unaigeukia Urusi na mamluki wa Kirusi kwa msaada.
Mnamo Januari, Ujumbe wa kujivunia wa Ufaransa, Takuba, unaoundwa na vikosi maalumu vya mataifa ya Ulaya kusaidiana na jeshi la Mali, ulikumbwa na mtafaruku baada ya kikosi cha Denmark kuambiwa kiondoke nchini Mali. Balozi wa Ufaransa nchini Mali pia alifukuzwa kufuatia vita vya maneno kati ya pande hizo mbili.
Soma pia: ECOWAS yaanza kutekeleza vikwazo vyake dhidi ya Mali
Huku hasira zikizidi kupanda, baadhi ya maafisa wa Ufaransa walisema hakuna chaguo zaidi ya kujiondoa kabisa kutoka Mali, ingawa mapambano mapana dhidi ya wapiganaji wa itikadi kali huko Sahel yataendelea.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian alisema Alhamisi iliyopita kuwa uamuzi juu ya mabadiliko na wanajeshi utafanywa ndani ya wiki, lakini hakutumia neno "kuondoa."
Kuondoka Mali, kitovu cha miaka mingi cha tishio kwa wanamgambo, inaweza kuwa na madhara makubwa, kuwaimarisha waasi ambao tayari waanahibiti maeneo makubwa, na kuchochea uhamiaji zaidi kutoka Afrika Magharibi kwenda Ulaya.
Pia ni tishio kwa washirika wa kimkakati wa kiuchumi wa Ufaransa kama Ivory Coast na Senegal. Wanadiplomasia na viongozi walieleza kuwa licha ya msuguano wa kisiasa, wanajeshi wa Ufaransa na Ulaya walikuwa bado wakifanya kazi na kuratibu vizuri kwa pamoja.
Soma pia: Mpango wa kuchelewesha uchaguzi wapingwa Mali
Mnamo Februari 8, jeshi la Ufaransa lilielezea kuhusu operesheni ya pamoja iliyohusisha ndege ya kivita ya Ufaransa, kikosi cha Takuba na Jeshi la Mali ambayo ilipelekea kuuawa kwa watu 30 wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Kiislamu.
Mwanadiplomasia moja wa Ulaya, alisema wakati akiisihi Paris kutoharakisha uamuzi, kwamba kuondoka kabisa litakuwa kosa, na kuongeza kuwa huwezi kuzungumza juu yake usalama katika Sahel bila kujikita Mali.
Kuelekea wapi?
Ni jambo gumu kwa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye anatarajiwa kugombea tena uchaguzi katika muda wa wiki chache zijazo, na anataka kutilia mkazo sifa zake za uongozi.
Ufaransa ilikuwa tayari imepunguza wanajeshi kutoka Sahel ikiwa na lengo la kupunguza idadi jumla kutoka karibu 5,000 hadi 2,500-3,000 ifikapo 2023. Karibu nusu ya vikosi vyake viko Mali, kwa hivyo Paris ingehitaji kuamua ni mahali gani pa kuviweka na kudumisha ufanisi wa kazi.
Soma pia: Mwanaume aliejaribu kumuuwa rais wa Mali afariki jela
Moja ya maeneo yenye uwezekano ni Niger, ambapo Paris tayari inaendesha ndege za kivita, ndege zisizotumia rubani. Waziri wa jeshi wa Ufaransa alitembelea mji mkuu wa nchi hiyo, Niamey mapema Februari, ili kujadili mabadiliko ya uwepo wa kijeshi wa Ufaransa kwenye kanda ya Sahel.
Lakini maafisa wa Niger katika miezi ya hivi karibuni wamekosoa wazo la kuongeza vikosi vya kigeni.
Soma pia: Mahakama ya Mali yamtangaza Goita rais wa mpito
Na wakati hisia za chuki dhidi ya Wafaransa siyo kubwa sana nchini Niger kama ilivyo katika nchi jirani ya Mali, bado zipo. Msafara wa kijeshi wa Ufaransa ulizuwiwa mwishoni mwa mwaka jana na askari wa Ufaransa walilaazimika kuyatua risasi huku ndege za kivita zikidondosha miako kuwaonya raia wanaozuia msafara.
Afisa mwandamizi wa kupambana na ugaidi nchini Niger hakuondoa uwepo wa Ufaransa, lakini alisema kulikuwa na mazingatio ya ndani ynayohitaji kufikiriwa, hasa baada ya mapinduzi ya kijeshi ya hivi karibuni nchini Burkina Faso, Chad na Mali.
Burkina Faso pia yaonekana ngumu
Vikosi maalum vya Ufaransa vinafanya kazi nje ya nchi hiyo, lakini mapinduzi ya Januari yameivuruga nchi hiyo. Uadui wa umma kuelekea Ufaransa ni dhahiri na utawala ya kijeshi lhaujaonyesha shauku ya kuendelea kushirikiana na kipindi cha karibu.
Soma pia: Umoja wa Mataifa waitaka Mali kufanya uchaguzi Februari
Kujiondoa Mali kunaweza kuchukua miezi kadhaa. Hilo lingeweza kutoa nafasi ya mazungumzo, hasa kama utawala wa kijeshi ungetafakari upya ratiba ya uchaguzi. Endapo vikosi vya Ufaransa vitaondoka hata hivyo, hili litazusha maswali kuhusu usalama wa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa MINUSMA wenye askari 14,000.
Kikosi cha 'A LA CARTE'?
Mfano wa kikosi kazi kilichopo cha Takuba cha Ulaya unaweza kuwa suluhisho moja.
Ujumbe huo unajumuisha nchi 14, nyingi zikiwa za Ulaya Mashariki na Scandinavia. Nguvu yake ardhini ya karibu 600-900 -inajumuisha timu za matibabu na usimamizi na kimekuwa kama kikosi cha kiishara zaidi kinachosindikiza vikosi vya ndani.
Soma pia: Mali yatangaza serikali mpya yenye maafisa wa kijeshi
Wakati kuna wasiwasi miongoni mwa baadhi ya mataifa ya Ulaya kuhusu mzozo wa kisiasa nchini Mali na uwepo wa Urusi na mamluki, wanadiplomasia wanasema hakuna haja ya kuiacha Paris peke yake, hasa katikati mwa mgogoro kwenye mipaka ya Ukraine, ambao umeyaacha mataifa ya kanda ya zamani ya mashariki yakitegemeana.
Maafisa wa Ufaransa wanaamini kuwa kikosi cha Takuba kinaweza kubadilishwa kupitia mfumo wa "la carte" ambapo nchi za Sahel na zaidi zinaweza kupata utaalamu, mafunzo au vifaa kutoka mataifa ya Ulaya.
Badala ya kuwa na maelfu ya wanajeshi walipelekwa tofauti na vikosi vya ndani, wangekuwa na uwepo wa siri kusaidia kuyaongoza majeshi hayo ya ndani.
Soma pia: AU yasitisha uwanachama wa Mali
"Sio juu yetu kuwalinda watu. Ni juu ya majeshi ya kitaifa kufanya hivyo. Kuanzia sasa tutawasindikiza. Mhimili wetu mpya wa ushirikiano ni kuyafanya majeshi ya Afrika kuwa huru zaidi," alisema afisa mwandamizi wa jeshi la Ufaransa.
Afisa mwandamizi wa ulinzi wa Ivory Coast alikubaliana na kauli hiyo, na kuongeza kuwa kulikuwa na mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea na Ufaransa huku ikitazamia kuirekebisha operesheni yake ya kukabiliana na ugaidi katika eneo hilo.
Msisitizo ni kuona jinsi operesheni zinaweza kubadilishwa ili kuyasaidia mataifa katika Ghuba ya Guinea, hasa Ivory Coast,Togo, Benin na Ghana, ambako kuna wasiwasi juu ya kusambaa kwa harakati za wapiganaji kutokana unywelevu wa mipaka, maafisa wa Ufaransa wanasema.
Mataifa ya Ghuba ya Guinea yameshuhudia mashambulizi ya hapa na pale na yalianzisha Mpango wa Accra, ambao ni ushirikiano wa kuzuia usambaji wowote kutoka kanda ya Sahel. Uimarishwaji wa mpango huo na msaada wa Ulaya unatazamiwa na baadhi kama jambo lenye uwezekano.
Lakini si kila moja ameshawishika. Mwanadiplomasia mmoja wa Ulaya aligusis unyeti wa kukaribisha askari wa kigeni, na kuongeza kwamba hawawezi kuhamishwa hamishwa tu kama vipande vya chess.
Chanzo: RTRE