1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU: Tufikirie mustakabali katika eneo la Ukanda wa Gaza

20 Novemba 2023

Wakati mapigano huko Gaza yakiendelea na raia wakiwa katika mzingiro, Umoja wa Ulaya inasisitiza 'kusimamisha'mapigano na kuwa na majadiliano.

https://p.dw.com/p/4ZEgZ
Brussels | Bunge la Umoja wa Ulaya likiwa katika kikao chake
Brussels | Bunge la Umoja wa Ulaya likiwa katika kikao chakePicha: Dwi Anoraganingrum/Future Image/IMAGO

Shambulio la Hamas kusini mwa Israel lililosababisha vifo vya watu 1,200 na watu wengine zaidi ya 200 kuchukuliwa mateka, ni hali iliyosabisha Israel kufanya mashambulizi makubwa ya kulipiza kisasi kwa zaidi ya wiki tano sasa.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa na wizara ya afya huko Gaza, yamesababisha vifo vya Wapalestina zaidi ya 11,000 huku wengine milioni 1.5 wakiyahama makazi yao.

Umoja wa Ulaya umetoa wito wa kusitishwa kwa muda mapigano huku ukianza kufikiria mustakabali wa eneo hilo. 

Mapigano makali yanayoendelea katika eneo dogo lenye wakazi wengi na linalodhibitiwa na Hamas la Gaza, yamesababisha hospitali nyingi kusitisha shughuli zake kutokana na uhaba wa nishati na vifaa vingine muhimu. Hayo ni kulingana na mashirika ya misaada eneo hilo.

Soma Pia:Palestina yasema hospitali ya kuhamishwa imeshafikishwa Gaza

Siku ya Jumatatu, shirika la Umoja wa Mataifa la kuwasaidia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limesema litalazimika kusitisha shughuli zake kwa muda wa siku mbili kutokana na ukosefu wa mafuta.

Lakini siku ya Jumatano(15.11.2023), tangu mzingiro kamili wa Israel, lori la kwanza lililobeba mafuta limefanikiwa kuvuka mpaka likitokea Misri na kuingia Gaza.

Hali tete ya kibinadamu Ukanda wa Gaza

Wakati mawaziri 27 wa Umoja wa Ulaya (EU) walipo kutana mjini Brussels siku ya Jumatatu, mkuu wa sera za kigeni wa Umoja huo Josep Borrell amesisitiza kuhusu wito wa pamoja wa kutaka usitishwaji wa muda wa mapigano ili kuruhusu ufikiaji wa misaada lakini hakutaja usitishaji kamili wa vita.

Ukanda wa Gaza | Wanajeshi wa Israel
Mzozo | Wanajeshi wa Israel wakiwa katika oparesheni GazaPicha: Israel Defense Forces/Handout/REUTERS

Borrell amewaambia waandishi wa habari kuwa takriban asilimia 10 tu ya mahitaji ya Gaza ndiyo pekee yaliyowasilishwa.

Umoja wa Ulaya ambao umekuwa ukitatizika kuwa na kauli moja juu ya mzozo huu wa Mashariki ya Kati, umetoa tamko la pamoja Jumapili jioni.

Katika taarifa hiyo, nchi wanachama wa EU zimetoa wito wa "usitishwaji mara moja na wa muda wa mapigano na kuanzishwa kwa njia salama za kibinadamu.

Viongozi hao wameamuru pia kuachiliwa kwa mateka waliosalia, lakini pia wakasisitiza kwa mara nyingine kuhusu haki ya kujilinda ya Israel chini ya sheria za kimataifa na sheria za kimataifa za kibinadamu.

Soma Pia:Uamuzi wa Afrika kusini kuipeleka Israel ICC- waibua mjadala

Mawaziri wa Umoja wa Ulaya wamelaani pia vitendo vya Hamas, ambayo EU, Marekani na mataifamengine wanaizingatia kama kundi la kigaidi, kwa matumizi ya hospitali na raia kama ngao.

Israel inalishutumu kundi hilo la wanamgambo kwa kujificha kwenye mahandaki ya miundombinu ya kiraia huko Gaza.

Migawanyiko katika usitishwaji kamili mapigano

Tamko hilo la pamoja ya Umoja wa Ulaya limetolewa baada ya Rais Emmanuel Macron kuijumuisha Ufaransa kwenye orodha ndogo ya nchi za Umoja wa Ulaya ambazo ni Uhispania, Ubelgiji na Ireland zinazotoa wito wa kusitishwa kikamilifu kwa mapigano na hivyo kusababisha ghadhabu kutoka kwa Israel.

Nchi nyingine za Ulaya kama Ujerumani, ambayoimekuwa ikiiunga mkono Israel tangu mashambulizi ya Hamas ya Oktoba 7, zimekataa kuunga mkono suala la usitishaji kamili mapigano wakisema hilo litainyima Israel haki yake kujilinda.

Kilio cha Waandishi Habari huko Gaza

Soma Pia:UN: Wakimbizi wa Kipalestina wanaishi katika mazingira duni

Siku ya Jumatatu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock ambaye alifanya ziara Mashariki ya Kati mwishoni mwa jumaa, amesema anasikitishwa na vifo vya wanawake na watoto wasio na hatia lakini akahojki kuhusu usalama wa Israel na hatima ya mateka zaidi ya 200.

Katika mkutano na waandishi wa habari kufuatia mkutano wa Jumatatu, Borrell alieleza kuwa ametoa pendekezo kwa mawaziri kuhusu seraya baadaye huku akitoa wito kwa EU kujihusisha zaidi katika mzozo huo hasa katika kile alichokiita "kuanzishwa kwa taifa la Palestina," huku akisisitiza kuwa Ulaya imekuwa ikijitenga na kuiachia Marekani jukumu la suluhisho katika mzozo kati ya Israel na Palestina.