Israel yaamrisha kuondolewa kila mmoja Al-Shifa
18 Novemba 2023Wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas katika taarifa imesema watu wengine 120 waliojeruhiwa bado wako katika hospitali hiyo pamoja na idadi ambayo haijawekwa wazi ya watoto waliozaliwa kabla ya muda wao.
Mapema maafisa wa afya wa Hamas waliliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa watu 450 waliojeruhiwa na wagonjwa mahututi hawakuweza kuondolewa na wanasalia katika hospitali hiyo pamoja na wahudumu wa afya wanaowahudumia.
Wakati huo huo, huduma za intaneti na simu zimerejeshwa ingawa si kikamilifu katika Ukanda wa Gaza, na kufikisha mwisho kipindi cha kukatika kwa mawasiliano kilichoupelekea Umoja wa Mataifa kusitisha uwasilishaji wake wa misaada muhimu kwa kuwa misafara yake ya magari haikuweza kuwasiliana.
Hayo yanafanyika wakati ambapo shambulizi la anga la Israel nje kidogo ya eneo la Khan Younis limesababisha vifo vya watu 26.