Waziri Mkuu wa Haiti Conille aelekea Marekani
29 Juni 2024Maafisa wa polisi ya Kenya waliopelekwa nchini humo wameanza kushika doria katika mji huo kama sehemu ya ujumbe unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa wa kupambana na magenge yenye silaha ambayo yamechukua udhibiti wa mji huo mkuu.
Ofisi ya Conille ilisema anasafiri na Waziri wa Mambo ya Kigeni Dominique Dupuy, Waziri wa Fedha Ketleen Florestal na mkuu wa utumishi Nesmy Manigat. Waziri wa sheria Carlos Hercule alibaki nchini ili kuhudumu kama kaimu waziri mkuu kwa niaba yake.
Ofisi hiyo ya waziri mkuu imesema ujumbe huo utakuwa na mikutano muhimu ya kazi na maafisa kutoka taasisi za fedha za kimataifa. Aidha utakagua ubalozi wa Haiti mjini Washington. Marekani ni mfadhili mkuu wa kikosi cha kimataifa cha usalama kinachoongozwa na Kenya ambacho kimeidhinishwa na Umoja wa Mataifa kupelekwa Haiti kusaidia polisi yake kupambana na magenge ambayo yameitumbukiza nchi hiyo katika mgogoro wa kibinaadamu.