SiasaHaiti
Kikosi cha polisi wa Kenya kuelekea Haiti Juni 25
24 Juni 2024Matangazo
Kenya ilijitolea kutuma takriban polisi 1,000 watakaoungana na vikosi kutoka nchi nyingine ili kusaidia kuleta utulivu nchini Haiti, lakini hatua hiyo ilikabiliwa na changamoto za kisheria katika taifa hilo la Afrika Mashariki.
Rais William Ruto amekuwa akiunga mkono hatua hiyo ambayo inatiliwa mashaka na shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch hasa kuhusu ufadhili wake.
Soma pia: Rais Ruto wa Kenya asisitiza kupeleka polisi nchini Haiti wiki chache zijazo
Mbali na Kenya, nchi nyingine ambazo zimeonyesha nia ya kujiunga na ujumbe huo wa kulinda amani Haiti ni pamoja na Benin, Bahamas, Bangladesh, Barbados na Chad.