Waziri Mkuu mpya wa haiti Conille aapishwa
4 Juni 2024Matangazo
Conille aliteuliwa na baraza la mpito la rais lililokuwa linaiendesha nchi hiyo kufuatia kuachia ngazi mnamo Aprili kwa Waziri Mkuu Ariel Henry, wakati ambapo machafuko yanayotokana na magenge yalipoongezeka.
Kuapishwa kwake sasa kunampa mamlaka ya kuunda serikali kwa kushauriana na baraza hilo.
Conille aliwahi kuhudumu kama waziri mkuu wa haiti kwa kipindi kifupi kati ya mwaka 2011 hadi 2012.
Soma pia:Waziri Mkuu mpya wa Haiti aahidi kutafuta umoja wa kitaifa
Machafuko yanayosababishwa na magenge yameizonga nchi hiyo na mwishoni mwa mwezi Februari makundi yaliyojihami yalifanya mashambulizi katika maeneo kadhaa ya kimkakati katika Mji Mkuu Port-au-Prince yakidai kwamba yanataka kumpindua Waziri Mkuu Henry.