1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa wajadili uchafuzi wa takataka za plastiki

29 Mei 2023

Kamati ya Umoja wa Mataifa inakutana hii leo huko Paris ili kushughulikia kile kinachokusudiwa kuwa mkataba wa kihistoria wa kukomesha uchafuzi utokanao na plastiki ulimwenguni.

https://p.dw.com/p/4Rvv8
Serbien | Umweltverschmutzung durch Plastik
Picha: Darko Vojinovic/AP/picture alliance

Kamati ya Umoja wa Mataifa inakutana hii leo huko Paris ili kushughulikia kile kinachokusudiwa kuwa mkataba wa kihistoria wa kukomesha uchafuzi utokanao na plastiki ulimwenguni.

Kamati hiyo ya majadiliano inayokutanisha wawakilishi wa serikali ina jukumu la kuendeleza mkataba wa kwanza wa kimataifa juu ya uchafuzi huo, unaofungamana kisheria ikiwa ni pamoja na mazingira ya baharini.

Mkutano huu ni wa pili kati ya mikutano mitano inayotarajiwa kufanyika ili kukamilisha mazungumzo hayo ifikapo mwishoni mwa mwaka 2024.

Binadamu huzalisha zaidi ya tani milioni 430 za plastiki kila mwaka, na kulingana na Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa, taka za plastiki zinazozalishwa duniani zinaweza kuongezeka mara tatu ifikapo 2060.