1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Ruto avunja baraza lake la mawaziri

11 Julai 2024

Rais wa Kenya William Ruto, amelivunja baraza lake la mawaziri na kumfuta kazi mwanasheria mkuu wa serikali, ikiwa ni sehemu ya hatua anazochukua kufuatia maandamano makubwa ya vijana wa kizazi cha Gen Z.

https://p.dw.com/p/4iBbz
Nairobi, Kenya | Rais William Ruto
Rais wa Kenya William Ruto Picha: TONY KARUMBA/AFP


Akihutubia taifa kupitia televisheni nje ya Ikulu ya Nairobi, Rais Ruto ameahidi kuunda serikali mpya ambayo itakuwa imara na yenye ufanisi. 

''Kulingana na mamlaka niliyopewa na ibara ya 1,521 na 1,525 B ya katiba na kifungu cha 12 cha sheria ya ofisi ya mwanasheria mkuu, nimeamua leo kuwafukuza kazi mara moja mawaziri wote na mwanasheria mkuu wa Jamhuri ya Kenya." Alisema.

Hata hivyo waziri kiongozi, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje, na bila shaka ofisi ya Naibu Rais haitaathiriwa kwa njia yoyote ile katika maamuzi hayo.

Soma pia:Rais Ruto aidhinisha marekebisho Tume ya Uchaguzi IEBC

Amesema amechukua uamuzi huo baada ya kusikiliza madai ya wananchi na kwamba atashiriki mara moja katika mashauriano ya kina katika sekta mbalimbali na mirengo ya kisiasa na Wakenya wengine, hadharani na binafsi, kwa lengo la kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Rais Ruto amesema hilo ni muhimu ili kuharakisha hatua madhubuti za kukabiliana na mzigo wa madeni, kuongeza rasilimali za ndani, kuongeza nafasi za ajira, na pia kupambana na ufisadi.