1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Buhari atangaza siku zaidi kurudisha fedha za zamani

16 Februari 2023

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari hii leo ametoa idhini kwa Benki kuu kuongeza muda wa kukamilisha urejeshwaji wa noti za zamani kwa siku 60 kufuatia uhaba wa pesa taslimu uliochochea ghadhabu kuelekea uchaguzi mkuu

https://p.dw.com/p/4NZjK
Nigeria | Godwin Emefiele und Präsident Muhammadu Buhari | Einführungszeremonie für neu gestaltete Banknoten
Picha: Sodiq Adelakun/Xinhua News Agency/picture alliance

Buhari amesema kwenye hotuba yake iliyorushwa kwenye televisheni kwamba noti ya zamani ya naira 200 itaendelea kutumika, pamoja na noti mpya za 1,000, 500 na 200 hadi Aprili 10. 

Matamshi yake yanakinzana na uamuzi wa muda uliotolewa na mahakama ya Juu ya wiki iliyopita, ya kwamba noti zote za zamani zitasalia "legal tender" hadi pale itakaposikiliza kesi zitakazowasilishwa na baadhi ya serikali za majimbo.

Soma pia:Uhaba wa mafuta na pesa taslimu vyatia doa kampeni ya uchaguzi Kaskazini mwa Nigeria

Baadhi ya wanasiasa wamekosoa hatua ya rais ya kutangaza wakati huu ambapo taifa hilo linajiandaa na uchaguzi, Februari 25, kwa kuwa kampeni zinafadhiliwa na fedha ambazo ni vigumu kufuatilia upatikanaji wake.