1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Uhalifu

Polisi Kenya yatangaza zawadi kwa muuaji alietoroka

22 Agosti 2024

Polisi nchini Kenya imetangaza zawadi ya pesa taslimu kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa za kuaminika zitakazowezesha kukamatwa kwa mshukiwa wa mauaji Collins Jumaisi aliyetoroka kutoka maabusu ya polisi mjini Nairobi.

https://p.dw.com/p/4jnhf
Kenya Nairobi | Dampo la Dandora
Miili kadhaa ya wanawake waliouawa ilikuwa kwenye dampo Nairobi, na mshukuwa wa mauaji hayo anadaiwa kuvunja gereza na kutoroka.Picha: Ben Curtis/AP Photo/picture-alliance

Polisi nchini Kenya imetangaza zawadi ya pesa taslimu kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa za kuaminika zitakazowezesha kukamatwa kwa mshukiwa wa mauaji Collins Jumaisi aliyetoroka kutoka maabusu ya polisi mjini Nairobi.

Idara ya upelelezi DCI hata hivyo haikutaja kiwango cha zawadi hiyo ya pesa.

Soma pia: Miili sita ya wanawake waliokatwa yakutwa dampo Nairobi

Je, Paul Mackenzie ana hatia ya kuua bila kukusudia?

Polisi ilianzisha msako siku ya Jumanne baada ya Collins Jumaisi, ambaye anatuhumiwa kwa mauaji ya wanawake kwa kuwakata vipande vya vipande, alitoroka kutoka kituo cha polisi cha Gigiri pamoja na raia 12 wa Eritrea.

Maafisa watano wa polisi waliofikishwa mahakamani jana kwa kushukiwa kumsaidia Jumaisi kutoroka, wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi 200,000 pesa za Kenya sawa na dola 1,500, licha ya waendesha mashtaka kutaka kuwaweka rumande kwa siku 14.