1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Mzozo wa Sudan hauna dalili za kumalizika

21 Julai 2023

Mzozo unaoendelea kwa miezi mitatu sasa nchini Sudan hauonyeshi dalili za kumalizika.

https://p.dw.com/p/4UDSD
FILE PHOTO: A Sudanese national flag is attached to a machine gun of Paramilitary Rapid Support Forces (RSF) soldiers as they wait for the arrival of Lieutenant General Mohamed Hamdan Dagalo before a meeting
Picha: Umit Bektas/REUTERS

Mapigano kati ya pande zinazozozana jana Alhamisi yamesababisha kukatizwa kwa muda kwa huduma za umeme na mawasiliano ya simu katika mji mkuu, Khartoum.

Soma pia: ICC yaanzisha uchunguzi kwa machafuko ya Sudan

Mapigano makali kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha dharura,RSF yameshuhudiwa hapo jana katika eneo kubwa la Sudan kuanzia Khartoum, Khartoum Kaskazini hadi Omdurman na kusambaa hadi mji wa Kodorfan Kaskazini, ulioko katikati ya Sudan.

Makabiliano hayo ya jana, yamesababisha kukatwa huduma za umeme, intaneti na mawasiliano kwa masaa kadhaa katika mji mkuu.

Soma pia: Watu 17 wauawa katika shambulizi la kutokea angani Khartoum

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu nchini Sudan imekuwa ikishirikiana na pande zinazopigana kwa matumaini ya kufikisha misaada zaidi ya kibinadamu katika eneo hilo lenye vita.