1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mji wa Khartoum watikiswa na miripuko kwa mara nyingine

4 Julai 2023

Kwa mara nyingine miripuko ilisikika katika mji mkuu wa Sudan Khartoum,jana Jumatatu wakati jeshi likiwataka raia kuchukuwa silaha kupambana dhidi ya mauaji yanayofanywa na wanamgambo wa RSF.

https://p.dw.com/p/4TO0l
FILE PHOTO: A Sudanese national flag is attached to a machine gun of Paramilitary Rapid Support Forces (RSF) soldiers as they wait for the arrival of Lieutenant General Mohamed Hamdan Dagalo before a meeting
Picha: Umit Bektas/REUTERS

Milio ya makombora imetikisa eneo la Kaskazini Magharibi mwa Khartoum na kuelekea eneo la kati na Mashariki mwa mji huo,kwa mujibu wa mashahidi waliozungumza na shirika la habari la AFP.

Mapigano makali pia yalizuka kwa muda wa saa kadhaa kati ya jeshi rasmi la serikali na wanamgambo hao siku ya Jumapili.

Jana Jumatatu jeshi likatangaza liko tayari kupokea na kuwaandaa wapiganaji wa kujitolea. Kauli ya jeshi imekuja baada ya Jumapili mkuu wa majeshi AbdulFatah al Burhani kuwatolea mwito vijana na watu wengine wenye uwezo wa kupigana kujiunga na jeshi.

Raia waliochoshwa na vita kwa kiasi kikubwa wamekataa wito huo, wakiomba kukomesha vita visivyokoma kati ya Burhan na makamu wake wa zamani, kamanda wa RSF Mohamed Hamdan Daglo.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW