SiasaItaly
Mkutano kati ya Meloni na viongozi wa Afrika waanza Rome
29 Januari 2024Matangazo
Serikali ya Meloni inataraji mpango wake huo utapunguza wimbi la wahamiaji,kutanua vyanzo vya nishati pamoja na kuanzishwa mahusiano mapya kati ya Ulaya na Afrika.
Viongozi wa juu kadhaa wa nchi za Afrika pamoja na Umoja wa Ulaya, Umoja wa Mataifa na wawakilishi wa taasisi za fedha za kimataifa wanashiriki mkutano huo wa Rome.
Hata hivyo mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat ameupokea kwa tahadhari mpango wa Italia kwa kuuambia mkutano huo wa kilele kwamba nchi za Afrika zingependelea zaidi kushauriwa kwanza kuhusu mpango huo kabla ya Italia kuuanzisha.
Faki ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu wa Chad ameuambia mkutano huo kwamba Waafrika hawafurahishwi na ahadi ambazo haziendelezwi.