1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MINUSMA:Zaidi ya watu 500 wameuwawa Mali

Hawa Bihoga
31 Mei 2022

Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya raia mia tano wameuwawa katika mashambulizi yaliofanywa baina ya vikosi vya kijeshi na vikundi vya itikadi kali kuanzia mwezi Januari hadi Machi 2022.

https://p.dw.com/p/4C6Wk
Mali | Proteste in Bamako
Picha: Ousmane Makaveli/AFP/Getty Images

Wakati mauaji hayo yakishuhudiwa haki zingine za binadamu zimerekodiwa kukiukwa kwa kiwango kikubwa licha ya nchi za magharibi kuwepo wananjeshi wake ili kulinda usalama dhidi ya makumndi ya kigaidi

Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa, MINUSMA, kilisema katika ripoti yake kwamba, wapiganaji kutoka katika vikundi vya itikadi kali vinasalia kuwa ni chanzo kikubwa katika cha ghasia dhidi ya raia na kuchochea ongezeko la kasi la vifo na ukiukwaji mwingine wa haki za binadamu.

 Unaohusishwa moja kwa moja na vikosi vya jeshi ambavyo vinaungwa mkono na vikosi vya kigeni.

Ripoti hiyo ya MINUSMA inaonesha kwamba idadi jumla ya watu waliouwawa katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2022 iliongezeka mara nne zaidi kutoka 128 mwaka 2021 hadi 543 mwaka 2022.

Soma zaidi:Serikali ya Mali yazuia jaribio la mapinduzi

Pande zote za mzozo ikiwa ni pamoja na wanajihadi,wanamgambo,kampuni binafsi ya ulinzi na hata vikosi vya usalama walihusishwa katika visa hivyo vya mauaji ya raia.

MINUSMA ilisema Jumla ya vifo 248 vya raia vilitokanana vikosi vya ulinzi na usalama na kurekodi visa 320 vya uvunjifu wa haki za binadamu.

Ripoti yaelekeza lawama kwa vikosi vya serikali

Mbali na mauaji ujumbe wa MINUSMA umesema vikosi vya usalama pia vinadaiwa kufanya ubakaji,uporaji na ukamataji wa kiholela wa raia wengi wakati wa oparesheni za kijeshi.

Operation Barkhane in Mali
Vikosi vya kulinda amani vikiwa katika majukumo yaoPicha: Philippe De Poulpiquet/MAXPPP/dpa/picture alliance

Ripoti inamulika kwamba ongezeko hilo ni mara kumi zaidi katika kipindi cha mwaka 2021 ambapo visa 31 pekee vilirekodiwahuku ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa ikielekeza lawama zaidi kwa vikosi vya serikali.

Ripoti hiyo haijaonesha moja kwa moja ni kwa namna gani majershi ya kigeni yalivyochangia kusaidia majeshi ya serikali.

Kwa upande wake shirika la kutetea haki za binadamu la Human Right Watch limesema kwamba wanajeshi wa Mali na wananjeshi wa Kigeni waliwanyonga karibu raia 300 huko Moura, katikati mwa nchi hiyo mnamo Machi 27 na 31.

Soma zaidi:Mali yaishtumu Ufaransa kwa ukiukaji wa anga lake kupeleleza wanajeshi

Mauaji hayo yaliofikia ongezeka la kiwango cha asilimi 324 kuliko kipindi cha robo mwaka uliopita yanatajwa kudhihirisha kushindwa kwa utawala wa kijeshi wa Mali katika kushughulikia vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu au kudhibiti shughuli za makundi yenye itikali kali yanayofungamana na Al-Qaeda na lile la dola la kiislam.

Mahusiano ya Mali na Urusi yatiliwa shaka kwa usalama wa raia

Utawala wa kijeshi wa Mali ulianzisha uhusiano wa karibu na Urusi na kuwaleta  wakufunzi wa kijeshi lakini Ufaransa ambayo ni mkoloni wa zamani wa Mali inashikilia kwamba ni mamluki wa kampuni ya kibinafsi ya ulinzi ya Wagner ambayo inahusiano wa karibu na Ikulu ya Kremlin.

Mali | MINUSMA | Hauptquartier in Bamako
Ujumbe wa MINUSMA ukiwa katika paredi ya kijeshi MaliPicha: Nicolas Remene/Le Pictorium/imago images

Uhusiano kati ya Mali na Ufaransa ulizorota vibaya kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya 2020 na hasa baada ya utrawala wa kijeshi uliotwaa madaraka kutangaza ratiba ya kurejesha democrasia ambayo mataifa ya magharibi yanasema haikubaliki.

Soma zaidi:Watu milioni 18 Ukanda wa Sahel kukabiliwa na baa la njaa

Mataifa ya Magharibi yanapinga vikali uingiliaji wa kampuni ya kibinafsi ya Wagner yakionya kwamba inaweza kuchochea vurugu nchini Mali na mataifa jirani ambako jamii zinakabiliwa na viwango vinavyoongezeka vya ukame, utapiamlo na hata umasikini.