UN: Wachunguzi wake wanazuiwa kuingia eneo la mauaji Mali
21 Aprili 2022Matangazo
Msemaji wa Umoja wa Mataifa Seif Majango amesema wapelelezi wa haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa bado hawajapewa idhini na mamlaka za Mali na kuwa muda unayoyoma ili kuhakikisha kuwa waliohusika wanawajibishwa kisheria na kuwapa haki wahanga.
Kwa mujibu wa Ripoti ya shirika la Human Rights Watch, inaaminika kuwa karibu wanaume 300 waliuawa kiholela na vikosi vya serikali na mamluki wa Urusi wakati wa shambulizi la Machi 27 hadi 30 katika mji wa Moura, ambao una wakaazi karibu 10,000 na umeingiliwa na wanamgambo wa itikadi kali.
soma zaidi: Baerbock atoa wito kwa Mali kuacha kushirikiana na Urusi
Mali ilikanusha madai hayo ikisema ilifanya operesheni halali ya kuwashambulia wapiganaji mjini Moura na kuwa itafanya uchunguzi wake yenyewe.