1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroItaly

Miili 14 ya wahamiaji yakutwa baharini

22 Juni 2024

Walinzi wa pwani ya Italia wamesema jana kwamba wamepata miili mingine 14 ya watu waliozama majini baada ya meli ya wahamiaji kuzama katika pwani ya kusini mapema wiki hii na kufanya idadi ya waliokufa kufikia 34.

https://p.dw.com/p/4hNel
Italia | Uhamiaji
Maua yakiwa yanaelea pembezoni mwa bahari kama alama ya kuwaaga wahanga wa ajali ya meli katika mkoa wa Calabria kusini mwa Italia, 2023Picha: GIANLUCA CHININEA/AFP/Getty Images

Zaidi ya watu 60 waliripotiwa kupotea baada ya mashua yao kuzama katika pwani ya Calabria usiku wa Jumapili, ambapo watu 11 waliokolewa.

Kulingana na walinzi hao wa pwani, msako wa angani na baharini bado unaendelea.

Shirika la Madaktari wasio na Mipaka lilisema mapema weiki hii kwamba boti hiyo ilikuwa inatokea Uturuki na kuzama karibu maili 120 kutoka pwani ya Calabria.