1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiItaly

Wahamiaji 11 wafa baharini, 60 hawajulikani waliko

18 Juni 2024

Watu 11 wamekufa na wengine zaidi ya 60 hawajulikani walipo, baada ya boti mbili zilizokuwa zimebeba wahamiaji kuanguka kwenye mwambao wa kusini mwa Italia.

https://p.dw.com/p/4hBJS
Kundi la misaada la Ujerumani RESQSHIP linaendesha uokozi.
Kundi la misaada la Ujerumani RESQSHIP linaendesha uokozi.Picha: Leon Salner/RESQSHIP e.V./dpa/picture alliance

Taarifa hii ni kulingana na makundi ya misaada, maafisa wa uokozi na mashirika ya Umoja wa Mataifa, siku ya Jumatatu.

Kundi la misaada la Ujerumani RESQSHIP linaloendesha boti ya uokozi ya Nadir limesema liliwaokoa hadi wahamiaji 51 kutoka kwenye boti ya mbao iliyozama, miongoni mwao, wawili walikuwa hawajitambui. Walikuta pia miili 10 iliyokwama chini ya boti hiyo. 

Boti ya pili ilianguka kilomita 200 mashariki mwa mkoa wa Calabria nchini Italia, baada ya kushika moto na kupinduka.

Boti hiyo ilikuwa ikitokea Uturuki, yamesema mashirika hayo na kuongeza kuwa watu 64 walipotelea baharini, na 11 waliokolewa.