Marekani yatangaza vikwazo kwa watu na makampuni chini Urusi
14 Septemba 2023Hivi ni vikwazo vikubwa zaidi kutangazwa na Marekani na idara za wizara ya fedha, na vya karibuni zaidi kuwalenga watu na makampuni ya mataifa mbalimbali na hasa Uturuki ambayo ni mwanachama mwenzake wa NATO ambayo huiuzia Urusi tekenolojia ya magharibi inayoweza kuchochea vita nchini Ukraine.
Soma pia:Marekani yaanza tena operesheni za kupambana na ugaidi Niger
Mkuu wa ofisi inayohusika na shughuli za uratibu wa vikwazo katika wizara ya mambo ya nje ya Marekani, James O'Brien ameliambia shirika la habari la AP kwamba vikwazo hivyo vinalenga kuzuia uendelezwaji wa sekta ya nishati nchini Urusi pamoja na vyanzo vya kifedha katika siku za usoni kama miradi ya gesi asilia ya Arctic, uchimbaji madini na uzalishaji na ukarabati wa silaha za Urusi.