SiasaMarekani
Marekani kuipatia Ukraine makombora ya masafa marefu
12 Septemba 2023Matangazo
Makombora hayo ni ya kisasa na yenye uwezo mkubwa.
Kwa muda wa miezi kadhaa, utawala wa Rais Biden umekuwa ukitatizika kuchukua uamuzi wa kutumwa kwa makombora hayo (ATACMS), kwa hofu kwamba usafirishaji wake ungelichukuliwa kama hatua ya uchokozi dhidi ya Urusi.
Lakini Ukraine imekuwa ikihimiza kupewa makombora hayo.
Soma pia:Marekani yaipa Ukraine msaada wa dola bilioni moja
Hadi sasa hakuna uamuzi wa mwisho uliofikiwa na haikuwa wazi ikiwa silaha hizo zingejumuishwa katika shehena ijayo ya msaada wa silaha kwa Ukraine.
Aina hiyo ya makombora imepigwa marufuku na zaidi ya nchi 100 lakini Urusi, Ukraine na Marekani hazikusaini Mkataba huo.