1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaionya Pyongyang ikiwa itaipatia silaha Urusi

6 Septemba 2023

Marekani imeionya Korea Kaskazini kwamba itakabiliwa na hatua kali ikiwa itaipatia Urusi silaha itakazozitumia kuwaua Waukraine.Urusi inaweza kuzitumia silaha hizo kushambulia miundombinu ya Ukraine.

https://p.dw.com/p/4W0Bm
Putin na Kim Jong Un
Rais wa Urusi Vladimir Putin na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un mwaka 2019Picha: Alexander Zemlianichenko/REUTERS

Marekani imeionya Korea Kaskazini kwamba itakabiliwa na hatua kali ikiwa itaipatia Urusi silaha itakazozitumia kuwaua Waukraine, huku ikiitolea wito wa kuheshimu wajibu wake wa kimataifa wa kutoisaidia Urusi kijeshi.

Mshauri wa masuala ya usalama wa taifa katika Ikulu ya White House Jake Sullivan amesema Urusi inaweza kuzitumia silaha hizo kushambulia miundombinu ya umeme na usambazaji wa vyakula wakati huu Ukraine inapoelekea majira ya baridi.

Sullivan ametoa onyo hilo, wakati kukiwa na uwezekano wa mkutano kati ya rais wa Urusi Vladimir Putin na kiongozi wa Korea Kaskazini kim Jong Un, hali inayoibua mashaka kuhusiana na matokeo ya ushirikiano baina ya mataifa hayo.