1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani kujadiliana na ICC juu ya uhalifu dhidi ya Putin

6 Septemba 2023

Ujumbe wa ngazi za juu wa bunge la Marekani unakutana na mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya makosa ya uhalifu, ICC juu ya uhalifu wa kivita dhidi ya rais wa Urusi, Vladimir Putin.

https://p.dw.com/p/4W1RG
ICC- Karim Khan
Mwendesha Mashitaka mkuu wa ICC Karim KhanPicha: EBRAHIM HAMID/AFP

Ujumbe wa ngazi za juu wa bunge la Marekani hii leo unakutana na mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya makosa ya uhalifu, ICC ya mjini The Hague kujadiliana juu yauhalifu wa kivita dhidi ya rais wa Urusi, Vladimir Putin.

Kiongozi wa ujumbe huo na mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mambo ya nje, Michael McCaul amesema atazungumza na mkuu huyo wa mashtaka wa ICC Karim Khan, ishara ambayo ni ya karibuni ya kuimarisha uhusiano baina ya Washington na ICC.

Kulingana na McCaul, watoto 30,000 wamechukuliwa kutoka kwenye familia zao na kupewa mafunzo nchini Urusi na Washington inaangazia namna ya kuisaidia mahakama hiyo kukusanya ushahidi zaidi ili kuthibitisha kesi dhidi ya Putin.

ICCilitoa waranti wa kumkamata Putin mnamo mwezi Machi kwa tuhuma za kuwachukua mamia watoto nchini Ukraine kinyume cha sheria, ingawa Urusi inakana madai hayo.