1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaitoa hofu Ukraine juu ya msaada wa kijeshi

20 Novemba 2023

Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amekutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na kumuarifu kwamba nchi yake itaendelea kuiunga mkono Ukraine kwa muda mrefu.

https://p.dw.com/p/4ZEfL
Diplomasia | Rais Volodymyr Zelensky na Waziri wa Ulinzi Marekani Lloyd Austin.
Diplomasia | Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akipeana mkono na Waziri wa Ulinzi Marekani Lloyd Austin.Picha: Ukrainian Presidential Press Office/AP/dpa/picture alliance

 Austin aliyefanya ziara ya ghafla mjini Kiev, amesema ujumbe aliokuja nao kwa kiongozi huyo ni kwamba Marekani iko pamoja naena itaendelea kuwa pamoja nae kadri itakavyohitajika. 

"Ujumbe niliokuletea mheshimiwa rais ni kwamba Marekani iko pamoja nawe na itaendelea kuwa pamoja nawe kwa muda mrefu." Austine alimuhakikishia rais Zelensky.

Soma pia:Marekani kuendelea kuiunga mkono Ukraine dhidi ya Urusi

Aliongeza kwamba kinachoendelea Ukraine hakiwahusu waukraine peke yao, bali kinaihusu dunia nzima, hivyo Marekani na washirika wake wataendelea kuipatia Ukraine kile inachohitaji kufanikiwa.  

Rais Zelensky aliisifu ziara ya Lloyd Austin akisema ni ishara nzuri kwa Ukraine, na kuishukuru Marekani kuinga mkono nchi hiyo pamoja na watu wake.  

Hii ni ziara ya pili ya Austin nchini Ukraine tangu Urusi ilipoanza uvamizi wake mwaka 2022.