1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lloyd Austin afanya ziara ya ghafla Ukraine

20 Novemba 2023

Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amefanya ziara ya ghafla mjini Keiv, leo kuihakikishia Ukraine kwamba nchi yake itaendelea kuiunga mkono katika vita vyake dhidi ya wanajeshi wa Urusi.

https://p.dw.com/p/4ZAny
Waziri wa Ulinzi Marekani Lloyd Austin akiwasili Kyiv leo
Waziri wa Ulinzi Marekani Lloyd Austin akiwasili Kyiv leoPicha: United States Secretary of Defense Lloyd Austin via X/REUTERS

Marekani imeendelea kuipa Ukraine mabilioni ya dola katika usaidizi wa usalama na kuahidi kuendelea pia kuiunga mkono nchi hiyo kadri itakavyohitajika. 

Hata hivyo wabunge wa upinzani wa chama cha Republican wameibua mashaka juu ya usaidizi wa Marekani kwa Ukraine katika siku za usoni. 

Soma pia:Kansela Olaf Scholz amtaka Putin kuondoa wanajeshi wake Ukraine

Wizara ya ulinzi ya Marekani,Pentagon imesema Austin atakutana na viongozi wa Ukraine kuzungumzia usaidizi wa kiusalama unaohitaji kwa taifa hilo kujilinda dhidi ya mshambulizi ya Urusi.

Hii ni ziara ya pili ya Austin nchini Ukraine tangu Urusi ilipoanza uvamizi wake mwaka 2022.