1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBurundi

Marais wa nchi wanacahama wa COMESA wakutana Bujumbura

31 Oktoba 2024

Marais wa nchi 21 wanachama wa Jumuia ya Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika, COMESA, wamepongeza hatua zilizopigwa na jumuia hiyo tangu ilipoanzishwa miaka 30 iliyopita.

https://p.dw.com/p/4mSTZ
Äthiopien Das Parlament in Addis Abeba
Picha: Minasse Wondimu Hailu/AA/picture alliance

Wakipokelewa na ngoma za asili kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa mikutano ni marais kutoka Kenya Wiliam Ruto, wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Felix Tschisekedi, Rais wa Zambia Hakainde Hichilema, wa Ethiopia, na Madagascar ambao wamehudhururia mkutano huo wa 23 wa COMESA. Eritrea na Somalia zimewakilishwa na waziri mkuu kutoka kila nchi.

Rais Ndayishimiye kwenye kiti wa sasa wa COMESA amesema kilimo kinachotumia na zaidi ya asilimia 80, ya raia wa nchi wachama wa COMESA kuna umuhimu kipewe kipaumbele ili kuweka msukumo kwenye ukuwaji kiuchumi ndani ya COMESA.

Kwa upande wake Rais wa Kenya William Ruto amesema kuna kila haja za kusheherekea miaka 30 ya uhai wa COMESA. Na kwamba Mikataba ya kibiashara na kimkakati iliimarishwa, na biashara iinayovuka mpaka kutoka nchi mmoja hadi nyingine ilirahisishwa. Isitoshi COMESA imekuwa na idadi kubwa ya raia wakikadiriwa kuwa milioni 640 na mtaji kwenye Benki ya TDB ukitoka kwenye trilioni moja na kufikia trilioni 40.

"Biashara kati ya nchi za COMESA ni kwa kiwango cha asilimia kumi pekee" 

Rais wa Kenya William Ruto
Rais wa Kenya William RutoPicha: BRYAN R. SMITH/POOL/AFP via Getty Images

Hata hivyo Rais Ruto amesema bado kuna changamoto ndani ya COMESA.

''Dola trilioni 40 ndani ya nchi 21 wanachama wa COMESA, tumefanya vizuri kweli, lakini tunaweza kufanya vizuri zaidi. Mikataba mingi ndani ya jumuia hiyo bado haijatekelezwa. Biashara kati ya nchi za COMESA ni kwa kiwango cha asilimia 10 wakati kwenye SADC ni asilimia 15 na kwenye Jumuia ya Afrika Mashariki ni asilimia 25.'', alisema Ruto.

Rais William Ruto naibu mwenyekiti wa COMESA ameagiza mabadiliko kwenye Umoja wa Afrika yaweze kufikiwa hivyo jumuia hiyo iachane na mfumo wake wa kuchukua maamuzi usiku wakati marais wamekwisha ondoka ukumbuni.

Kina cha maji chaongezeka katika ziwa Tanganyika

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat amezitaka nchi wanachama wa COMESA kusaini sheria inayoagiza uhuru wa watu na bidhaa Afrika.

''Huwezi kufanya biashara pasina kuwepo na uhuru wa watu na bidhaa, COMESA inalo jukumu kubwa kuhakikisha hatua hiyo ndani ya nchi wanachama wake. Na Umoja wa Afrika ulianzisha mchakato wa kufanya mabadiliko katika taasisi zake na kazi hiyo ilikabidhiwa kwanza Rais Paul Kagame wa Rwanda na baadaye kupewa Rais Wiliam Ruto.'', alisema Faki.

Miongoni mwa maagizo ya mkutano huo Rais Ndayishimiye ameahidi kuondoa malipo ya visa kwa raia wote kutoka nchi za COMESA wanaoingia Burundi.