Hamas na Houthi wajadili kutanua makabiliano na Israel
16 Machi 2024Shirika la habari linaloiunga mkono Iran Al Mayadeen, limeripoti kuwa maafisa wakuu wa Hamas, wanamgambo wa Islamic Jihad na kundi linalopigania ukombozi wa Palestina walihakikishwa na Wahouthi kwamba wataendelea na hujuma katika bahari ya Sham licha ya mashambulizi ya anga ya Marekani na Uingereza.
Mkutano huo, ambao ukumbi wake haukuwekwa wazi, ulikuwa sehemu ya kujiandaa kwa uwezekano wa kuongezeka kwa mzozo na mashambulizi zaidi ya Israel katika mji wa Rafah ambapo zaidi ya Wapalestina milioni moja wamekimbilia kutafuta hifadhi.
Soma pia: Malori ya misaada ya WFP yawasili Gaza
Waasi wa Houthi wamekuwa wakizishambulia meli katika bahari ya Sham na ghuba ya Aden katika kile wanachosema ni kuonyesha mshikamano kwa Wapalestina.
Hata hivyo, hakukuwepo na kauli yoyote kutoka makundi hayo manne kuhusu mkutano huo.