You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Sauti zetu
Vidio zetu
Yanayoangaziwa
Uchaguzi wa Marekani 2024
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Matangazo
Picha: Zoonar/picture alliance
Picha: Zoonar/picture alliance
Makala zetu
Sikiliza makala kemkem tulizokuandalia
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Msigwa: Chadema imepoteza mwelekeo wake wa kisera
Kambi ya upinzani nchini Tanzania imepata pigo kubwa baada ya mwasiasa mkongwe wa upanzani mMchungaji Peter Msigwa kutimkia chama tawala CCM huku akitangaza chama chake cha zamani kukosa mwelekeo katika masuala kadhaa ikiwemo demokrasia na mwelekeo wa kisera, lakini anakoselewa kuwa ni mwanasiasa mwenye uchu wa madaraka. Msikilize akijibu tuhuma hizi
Vikosi vya Tanzania vitaendelea kubaki Msumbiji
Katika wasaa huu wa takriban dakika kumi Sudi Mnete anazungumza na waziri wa Ulinzi nchini Tanzania Stergomena Tax kutaka kujua mwenendo wa oparesheni ya kijeshi ya vikosi vya Tanzania nchini Msumbiji.
Waasi wa M23 wakanusha kushirikiana na jeshi la Rwanda
Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wa M23 wameweka chini mtutu wa bunduki ili kupisha misaada ya kiutu kuingia katika maeneo yanayoshuhudia mapigano makali. Hatua hii inafanyika katika wakati ambapo Rwanda inashutumiwa kupeleka vikosi vyake kupigana mashariki mwa Kongo, je Kigali inaunga mkonoM23?. Katika Kinagaubaga sikilize msemaji wa M23
Umasikini unavyowatesa wastaafu Germany
Mstaafu mmoja kati ya watano nchini Ujerumani anakabiliwa kuwa katika hatari ya umasikini, kulingana na ofisi ya takwimu ya Ujerumani. Idadi ni kubwa zaidi hasa kwa upande wa wanawake
Akili mnemba katika soka
Makala ya Sema Uvume leo inamulika namna akili mnemba inavyotumika na inavyotarajiwa kutumika katika maeneo mbalimbali ya mpira wa miguu.
Mabadiliko ya uongozi kwenye Jumuiya ya kijeshi ya NATO
Kwa mujibu wa taarifa, Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte, anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa jumuiya ya kujihami ya NATO baada ya mpinzani wake rais wa Romania Klaus lohannis, kujoindoa kwenye kinyangànyiro. Mtayarishaji Zainab Aziz
Kujikolonisha kwa wasomi wa Kiafrika
Mohammed Khelef anazungumza na Profesa Mutembei juu ya dhana ya "kujikolonisha" miongoni mwa wasomi wa Kiafrika.
Raia wa Sudan wakabiliwa na madhila ya vita
Raia wa Sudan wanakabiliwa na usalama mdogo, ukosefu wa chakula, maji safi na huduma nyingine muhimu.
Masuluhisho kupitia habari
Mjadala juu ya nafasi ya vyombo vya habari vya Afrika kusaka masuluhisho ya matatizo ya Kiafrika.
Ipi hatima ya Ulaya baada ya uchaguzi wa bunge la Ulaya?
Katika Maoni mbele ya Meza ya Duara, Mohammed Khelef amewashirikisha wadau kadhaa kuzungumzia mafanikio yaliyopatikana kwa vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia katika uchaguzi wa bunge la Ulaya.
Matokeo ya Uchaguzi wa Bunge la Ulaya
Uchaguzi wa Bunge la Ulaya ulifanyika kuanzia tarehe 6 hadi 9 Juni 2024 katika jumla ya mataifa 27 ya Umoja huo. Matokeo ya uchaguzi huo yalikuwa pigo kubwa kwa vyama vya jadi, kutokana na vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia na vile vya kizalendo kupata matokeo mazuri. Hata hivyo vyama vya kihafidhina vilishinda uchaguzi huo. Ungana na Bakari Ubena katika kipindi hiki cha Mwangaza wa Ulaya.
Germany inakabiliana vipi na uhalifu wa ukoloni Tanzania?
Ujerumani bado inaendeleza juhudi zake za kujivua gamba na yaliyotokea katika kipindi cha ukoloni nchini Tanganyika ambayo ni Tanzania bara ya sasa, mafuvu kadhaa ya binadamu walionyongwa yalisafirishwa kutoka nchini humo hadi Ujerumni kuhifadhiwa. Sasa familia za wahusika wameweka madai mezani. Sikiliza mahojiano.
Unafahamu kumudu kuongea lugha zaidi ya tatu ni mtaji?
Wataalamu mbalimbali wanasema watu wengi duniani wanaweza kumudu kuzungumza walau lugha zaidi ya mbili kwenye maisha yao duniani. kufahamu lugha kunatajwa kuwa ni nyenzo muhimu kwako kijana kufungua fursa. Je unaongea lugha ngapi?
ANC yakosa wingi wa kura kuweza kulidhibiti Bunge
Zainab Aziz amewakaribisha wachambuzi kukijadili chama cha ANC kinacholazimika kuunda serikali ya mseto.
Masharti yapunguzwa kwa wanaotafuta kazi Germany
Mnamo Juni Mosi Ujerumani ilianza kutumia rasmi sheria mpya ambayo inawaruhusu watu wenye ujuzi kutoka mataifa ambayo hayapo ndani ya Umoja wa Ulaya, kuingia nchini humo na kutafuta ajira. Sheria ambayo inatajwa kuwa itapunguza changamoto ya uhaba wa wafanyakazi katika kada mbalimbali kwenye taifa hilo la Ulaya.
Watu wa nje ya Umoja wa Ulaya kufanya kazi Germany
Sura ya Ujerumani na Sheria mpya ya kuwaruhusu watu kutoka nje ya Umoja wa Ulaya kuja kufanya kazi Ujerumani.
Jukwaa la Manufaa
Angela Mdungu anakupa nafasi ya kutoa dukuduku pongezi, maoni au ushauri kuhusu masuala yanayohusu jamii inayokuzunguka.
Kinagaubaga: Athari za mradi wa SGR kwa watu wa Mombasa
Kadara Swaleh kutoka nchini Kenya anachambuwa athari za mradi wa reli ya SGR kwa wakaazi wa Mombasa.
Makala ya Karibuni ya 01.06.2024
Katika makala ya Karibuni mgeni wetu Gervas Lukada, mwanafunzi wa Kitanzania mwanataaluma ya mionzi anaishi Hamburg.
Vijana na muenendo wa kujitoa wenyewe
Katika makala hii ya Vijana mchakamchaka, tunamulika muenendo wa kizazi maarufu cha Gen Z, wa kujitoa chenyewe bila wenza, au wapenzi. Kwa nini mtindo huu umeshika kasi sana? Nini kinawafanmya vijana kutaka kuwa na kile wanachoita “me time“ yaani kujitengea muda wao?
Miaka 75 ya katiba ya Ujerumani
Katiba ya Ujerumani iliyoundwa na kuanza kutumika Mei 23 mwaka 1949 sasa imetimiza miaka 75. Sikiliza hapa makala ya Sura ya Ujerumani inayoimulika katiba hiyo Kongwe.
25.05.2024: Matangazo ya Mchana
Kwenye Matangazo ya Mchana utasikia pamoja na mengineyo taarifa ya habari za ulimwengu na makala ambazo ni pamoja na mjadala mrefu na wa kina wa Maoni kuhusiana na kifo cha ghafla cha aliyekuwa Rais wa Iran Ebrahim Raisi. Utasikia mengi kuhusu kiongozi huyo na kile kinachotarajiwa nchini humo baada ya kifo chake. Ungana nasi hapa.
Rais wa Kenya William Ruto apendekeza kupandisha kodi
Zainab Aziz amewakaribisha mezani wachambuzi kuzungumzia mapendekezo ya kupandisha kodi nchini Kenya.
TCRA na usimamizi wa vituo vya habari Tanzania
Katika makala hii Mohammed Khelef ameketi chini na meneja wa huduma za utangazaji Andrew Kisaka kutoka Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA na kuzungumzia namna mamlaka hiyo inavyosimamia vyombo vya habari vya utangazaji Tanzania na hatua wanazozichukua pale vinapokiuka kanuni.
Namna akili ya kubuni AI inavyotumiwa kuwarubuni watu
Hapo awali matapeli walitumia ujumbe au barua pepe kufanya ulaghai lakini sasa wamegeukia teknolojia ya AI kutapeli.
Athari za mafuriko nchini Tanzania
Makala Yetu leo inaangalia athari zilizotokana na mvua kubwa zilizonyesha na kusababisha mafuriko makubwa Tanzania.
Marafiki kupostiana mtandaoni siku ya "Birthday"
Utamaduni wa kusheherekea siku ya kuzaliwa umebadilika hasa katika zama hizi za kidigitali na kupostiwa mtandaoni.
Wafungwa wanaosalia jela Burundi baada ya kumaliza vifungo
Ni kwa nini mfungwa asalie gerezani hata baada ya kumaliza kifungo chake? Ndilo swali ambalo makala ya Mbiu ya Mnyonge inaangazia kule nchini Burundi. Na je wanaofungwa kinyume cha sheria watapataje haki? Mtayarishaji wa makala ni Amida Issa akiwa mjini Bujumbura, Burundi.
Makamu wa Rais wa Zanzibar azungumzia umoja wa kitaifa
Wakati hatima ya ushiriki wa mshirika mdogo kwenye serikali ya umoja wa kitaifa visiwani Zanzibar, chama cha ACT Wazalendo, ikining'inia baina ya kubakia na kutoka, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa chama hicho, Othman Masoud Othman, anazungumza na Mohammed Khelef wa DW kuhusu uhalisia wa mambo ulivyo.
Nafasi ya Tanzania katika uwanja wa kidiplomasia
Katika Makala ya Kinagaubaga, Mwenzetu Florence Majani amezungumza na Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa nchini Tanzania January Makamba, juu ya mambo mengi likiwemo hili la nafasi ya taifa hilo la Afrika Mashariki katika uwanja wa kidiplomasia.
Joel Nanauka katika Kinagaubaga na DW Kiswahili
Joel Nanauka kutoka Tanzania ni mwandishi wa vitabu na msomi aliyebobea katika masuala ya Diplomasia na uchumi na ni miongoni mwa vijana wenye ushawishi zaidi barani Afrika, kwa kuielimisha jamii hasa vijana kuhusu mambo yasiyofundishwa katika mfumo rasmi wa elimu ya darasani. Veronica Natalis amezungumza ne katika Kinagaubaga.
Ujerumani yakabiliwa na uhaba mkubwa wa makazi
Uhaba wa makazi nchini Ujerumani, ni tatizo kubwa la kijamiii. Kupata nyumba ya kupanga hivi sasa limekuwa suala gumu ambalo linaweza kufananishwa na kushinda bahati nasibu. Ungana na Angela Mdungu katika makala ya Sura ya Ujerumani kufahamu zaidi kuhusu tatizo hilo.
Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania
Mohammed Khelef anaongoza Meza ya Duara kujadili miongo sita ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mikopo ya mitandaoni na chungu yake
Matangazo ya mikopo ya mitandaoni huwavutia watu kwasababu ya masharti yake nafuu. Lakini namna ya kudai madeni inatajwa kudhalilisha wadaiwa. Ungana na Florence Majani, katika makala yetu leo.
Ujerumani kulifanyia mageuzi jeshi lake
Makala ya Sura ya Ujerumani leo inaangazia mpango wa Waziri wa Ulinzi Boris Pistorius wa kulifanyia marekebisho jeshi la nchi hiyo, "Bundeswehr". Maheuzi hayo yanatokana na kile anachokiita Pistorius kuwa kitisho cha kiusalama barani Ulaya.
Miaka 30 tangu mauaji ya Kimbari ya Rwanda
Rashid Chilumba anaongoza kipindi cha Maoni kujadili miaka 30 tangu kutokea mauaji ya kimbari nchini Rwanda.
14.04.2024: Matangazo ya Mchana
Kwenye Matangazo ya Mchana utasikia Taarifa ya habari za ulimwengu, makala ya Afrika Wiki Hii inayijumuisha mambo yaliyogonga vichwa vya habari kote barani Afrika pamoja na kipindi kizuri kabisa cha salaamu na muziki. Ungana nasi hapa kusikiliza zaidi.
06.04.2024: Matangazo ya Mchana
Matangazo ya Mchana, yanasikika hapa. Utasikia Taarifa ya Habari ambako kuna mengi yanayogonga vichwa vya habari duniani. Lakini pia kuna Maoni mbele ya Meza ya Duara, ambapo wafuatiliaji wanamchambua, Waziri Mkuu mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na changamoto zinazomkabili. Karibu.
Utafutaji Abaya na uchoraji heena ni miongoni mwa maandalizi ya Eid-Ul Fitr
Wikendi ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani waislamu wako kwenye ibada za mwishoni lakini pia kwenye maandalizi ya sherehe za Eid Ul Fitri. Heka heka za kutafuta Abaya za Eid zimepamba moto. Jiunge na Saumu Mwasimba amekuandalia uhondo kuhusu uchoraji heena huko Zanzibar na shamrashamra zilizotawala huko Burundi kuelekea Eid,katika makala ya Karibuni
DR Congo yapata Waziri Mkuu Mwanamke
Je Rais Tshisekedi amemchagua Judith Suminwa Tuluka kwa sababu ni mtu wake wa karibu au ni kutokana na uwezo alionao?
Habineza na hali ya upinzani Rwanda
Frank Habineza anazungumza juu ya hali ya kisiasa katika taifa hilo dogo la Afrika Mashariki.
Ulaghai wa wawekezaji wa Kigeni Afrika
Katika makala yetu leo, Emmanuel Lubega anazungumzia msamaha wa kodi wanaopewa wawekezaji wa kigeni barani Afrika kwa muda fulani wakati wanapoanzisha shughuli zao. Hata hivyo suala hilo linapingwa vikali na wachumi barani Afrika.
Sema Uvume: Programu inayosaidia wasioona kutumia mitandao
Programu maalum za kuwasaidia wenye ulemavu wa macho kutumia majukwaa hayo zimeanza kufanya kazi.
Tabia za vijana wakati wa miezi ya toba
Lilian Mtono anazungumza na vijaa haswa kuhusu kubadilisha mienendo ya kimaisha, wakiachana na maovu, kuwa watii, wanyenyekevu na kufanya ibada zaidi. Lakini ni kwa bahati mbaya kwamba wengi hurejea kwenye mienendo ileile ya kimaisha ya kabla ya kipindi kama hiki cha toba.
Hali ya makazi mijini Afrika Mashariki
Kwenye Makala Yetu Leo, tunaangazia hali ya makazi katika miji kwenye ukanda wa Afrika Mashariki. Shirika la makazi la Umoja wa Mataifa, UN-Habitat, linasema idadi ya wakazi wa mitaa ya mabanda inatazamiwa kufikia bilioni 3 ifikapo mwaka 2050 huku mzozo wa makazi ukizidi kuwa mkali duniani.
Huduma za serikali ya Zanzibar mtandaoni
Mwandishi wa DW Salma Said anazungumza na Mkurugenzi mtendaji wa serikali mtandao kutoka Zanzibar, kuhusu uendeshaji wa shughuli za serikali na huduma kwa njia ya mtandao. Kufahamu mengi sikiliza mahojiano kamili.
Nafasi ya chama cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania
Rashid Chilumba anaongoza kipindi cha Maoni kutathmini nafasi ya chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania.
Miaka 13 tangu kutokea ajali ya Fukushima
Ajali ya Fukushima inazingatiwa kuwa janga la pili la nyuklia katika historia ikilinganishwa na janga la Chernobyl.
Kauli ya Papa Francis yazua hisia mseto
Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amesema katika mahojiano kwamba Ukraine inapaswa kuwa na kile alichokiita ujasiri wa kupeperusha "bendera nyeupe" kama ishara ya kusalimu amri na kukubali kufanya mazungumzo ya kumaliza vita na Urusi. Kauli hiyo imeichukiza mno Ukraine na washirika wake wa Magharibi.
Madhara ya kiafya kwa madereva wa bodaboda
Makala ya afya yako Deo Kaji Makomba kutoka makao makuu ya Tanzania, Dodoma, anaangazia madhara ya kiafya wanayoweza kuyapata madereva wa pikipiki maarufu kama boda boda ambao hujishughulisha na shughuli za usafirishaji abiria katika maeneo mbalimbali nchini humo.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 2 wa 3
Ukurasa unaofuatia