You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Sauti zetu
Vidio zetu
Yanayoangaziwa
Uchaguzi wa Marekani 2024
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Matangazo
Picha: Zoonar/picture alliance
Picha: Zoonar/picture alliance
Makala zetu
Sikiliza makala kemkem tulizokuandalia
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Mfumo wa kidijitali wa matumizi ya maji
Maji Smarti ni mfumo wa kielektroniki unaowezesha kutoa taarifa za kiwango cha maji kilichopo katika chanzo husika, pamoja na kugundua kama kuna uharibifu wa miundombinu ya maji. Mfumo huu umetengenezwa na wanafunzi wa kidato cha sita kutoka Shule ya Sekondari ya Arusha Sayansi, iliyoko kaskazini mwa Tanzania, na tayari umeanza kutumika shuleni hapo.
Unalijua tatizo la Shoulder impingement Syndrome?
shoulder Impingement Syndrome inatokea pale mifupa katika bega lako inaposuguana au kubana katika misuli, na kufanya sehemu hiyo kuwa na maumivu makali. Makala ya Afya Yako inaliangazia zaidi tatizo hilo pamoja na tiba yake.
Fahamu zaidi kuhusu ugonjwa wa Parkinson
Parkinson ni ugonjwa unaoathiri mfumo wa neva katika ubongo, na kusababisha harakati zisizodhibitika kama vile kutetemeka, kukakamaa kwa misuli, na ugumu wa kusawazisha mwili. Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), ugonjwa wa Parkinson umeongezeka mara mbili katika miaka 25 iliyopita, na kufikia zaidi ya milioni 8.5 duniani. #kurunziafya 11.11.2024
Kinagaubaga: Masoud Kipanya azungumzia harakati zake
Katika makala hii Anuary Mkama anazungumza na mjasiriamali na mchora katuni maarufu nchini Tanzania Masoud Kipanya.
05.11.2024: Matangazo ya asubuhi
Sikiliza matangazo ya asubuhi ya DW Kiswahili
04.11.2024: Matangazo ya asubuhi
Sikiliza matangazo ya asubuhi ya DW Kiswahili
Kwanini Lesotho ndio nchi yenye baridi kali Afrika?
Lesotho ndio nchi inayotajwa kuwa na baridi kali Afrika. Kila mwaka theluji huanguka nchini humo, na wakati mwingine mapema kuliko ilivyo kawaida. Tizama vidio ifuatayo kwa ufahamu zaidi. #77asilimia
Vifaa duni vyaathiri huduma kwa wenye magonjwa ya damu
Jukwaa la Viongozi wa magonjwa ya damu limefanyika huku miundombinu duni ya afya, ukosekanaji wa wataalamu wa afya na upungufu wa vifaa tiba vikitajwa kuwa ndicho chanzo cha matibabu na usimamizi duni kwa wenye magonjwa ya damu, Afrika Mashariki. Mwenzetu Florence Majani alihudhuria jukwaa hilo na kutuandalia taarifa hii.
Vijana wanaougua saratani waongezeka, Kenya
Wataalamu hawa wanasema kiwango kikubwa cha vijana waathirika ni wenye umri kati ya miaka 12 hadi 25.
Kinagaubaga kwa ripoti ya HRW na majibu ya Profesa Kabudi
Kinagaubaga kuhusu ripoti ya Human Rights Watch kwa Tanzania na majibu ya Waziri wa Katiba na Sheria Palamagamba Kabudi.
24.10.2024: Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Miongoni mwa habari tulizonazo asubuhi hii ni Ujerumani na Austria zawaita mabalozi wa Korea Kaskazini kufuatia tuhuma za kuwapeleka wanajeshi wake nchini Urusi. Ufaransa yanuia kukusanya dola milioni 540 kwa ajili ya kuisaidia Lebanon na Watu watano wauawa na wengine 22 kujeruhiwa katika shambulizi kwenye kiwanda cha vifaa vya ndege nchini Uturuki. Ungana nasi.
Mapambano dhidi ya ufisadi Kenya
EACC Kenya inawachunguza maafisa 67 wa ngazi za juu katika kaunti, ikiwa ni sehemu ya kesi 231 za ufisadi zinazoendelea
Mwangaza wa Ulaya: Athari za utalii uliokithiri Barcelona
Jiji la Uhispania la Barcelona ni lenye historia ya kipekee, hali ya hewa ya joto na fukwe za kupendeza. Lakini sifa zote hizi zimeifanya Barcelona kuwa kivutio kwa mamia ya maelfu ya wageni na hivyo kuathirika na viwango vya juu vya utalii. Idadi ya watalii wanaoutembelea mji huo inazidi kuongezeka na hivyo kuchochea hasira miongoni mwa wenyeji wanaolalamika kwamba mambo mengi yamebadilika.
Mwalimu Nyerere, kiongozi adimu mwenye maono
Mnamo wiki hii Watanzania wamemkumbuka kiongozi wao adhimu, Mwalimu Julius Nyerere aliyeaga dunia miaka 25 iliyopita baada ya kuwaachia watanzania na waafrika kwa jumla turathi za milele: uhuru wa Tanganyika, Muungano wa Tanzania, Umoja wa nchi za Afrika,OAU na ukombozi wa kusini mwa Afrika. Wataalamu wetu wameyajadili hayo na mengine mengi kwenye meza ya duara.
Chanjo ya mpox kuchukuwa muda mrefu zaidi Kongo
Kongo imetakiwa kuchukuwa juhudi kubwa za kujenga ufahamu wa watu kuhusu virusi vya mpox na upatikanaji wa chanjo.
Changamoto na mchango wa wanawake vijijni katika maendeleo
Siku ya Wanawake wa vijijini inaadhimisha mchango wa kundi katika maendeleo na ustawi wa dunia.
Matangazo ya asubuhi: 14.10.2024
Sikiliza matangazo ya asubuhi ya DW Kiswahili
Mfahamu msichana mwalimu wa biashara
Salma ni msichana wa miaka 22 ambaye amekuwa akiwafundisha vijana namna ya kuanzisha biashara na kuziendeleza. Hata hivyo, si rahisi kwa baadhi yao kumuelewa lakini bado anamatumaini makubwa ya kufikia kundi kubwa la vijana, ili kuhakikisha kuwa wanajikwamua katika ajira na kuishi katika ndoto zao. #msichanajasiri.
Uwezo wa dawa za kiasili na usalama wake Kenya
Wagonjwa zaidi wanaougua magonjwa sugu wanaripoti hali yao ya kiafya kuimarika baada ya kugeukia dawa za kiasili. Wadau kwenye sekta hii wanasema kuna haja ya kuwianisha dawa za kiasili na za kisayansi ili kuupiga jeki mfumo wa afya nchini Kenya. Makala ya afya yako hii inajikita kwenye mada hii na mwandishi na msimulizi ni Wakio Mbogho.
Ukiukaji wa haki za binadamu Kenya
Serikali ya Rais aliyeko madarakani Kenya William Ruto inakosolewa kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu miaka miwili tangu ilipoingia madarakani. Zaidi ya mauaji 128 ya kiholela yamerekodiwa na visa 351 vya unyanyasaji kuripotiwa na mashirika ya kutetea haki za binadamu tangu mwaka 2022. Wakio Mbogho anajikita kwenye suala hili katika makala hii ya Mbiu ya Mnyonge.
Saidi Nguba "Edward Moringe Sokoine: Maisha na Uongozi wake"
Hivi karibuni kumefanyika uzinduzi wa kitabu cha Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine: Maisha na Uongozi wake.Kitabu hicho kimezungumzia maisha ya kiongozi huyo na urathi wa kisiasa na kiuongozi aliowaachia Watanzania. Kitabu hicho kilichoandikwa na waandishi nguli wa habari Salva Rweyemamu na Saidi Nguba. Rashid Chilumba alipata fursa ya kuzungumza na Nguba, msikilize.
Mabadiliko katika tamasha la Oktobafest nchini Ujerumani
Sura ya Ujerumani wiki hii inaangazia Halfa ya kila mwaka, maarufu kwa jina la tamasha la oktoba, (Oktoberfest) katika jimbo la Bavaria, kusini mwa Ujerumani, lililomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kongo kuanza kampeni ya chanjo ya mpox mkoani Kivu Kaskazini
Waziri wa afya wa Kongo amesema lengo la kampeni hiyo ni kuwapa chanjo watu walio katika hatari zaidi.
Makala: Wakimbizi wa ndani wageukia kilimo Kongo
Benjamin Kasembe anaangalia jinsi wakimbizi waliopo mjini Goma wanavyoendeleza kilimo kama njia ya kujikimu kimaisha.
Mwangaza wa Ulaya: Chama cha FPÖ chashinda uchaguzi Austria
Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia kinachojinasibu cha uhuru wa Austria FPÖ, kimeibuka mshindi kwa kujipatia asilimia 29.2 ya kura kwenye uchaguzi wa Bunge uliofanyika katika taifa hilo la Ulaya lenye watu milioni 9. Kiongozi wa chama hicho na waziri wa zamani wa mambo ya ndani wa Austria Herbert Kickl ameutaja ushindi huo kuwa wa kihistoria.
Fahamu namna ya kujenga uelewa kuhusu kuzuwia kujitoa Uhai
Kulingana na takwimu za shirika la afya ulimwenguni WHO, zaidi ya watu laki saba hukatisha uhai wao kila mwaka kwa kudhamiria. Je ni nini hasa kinamfanya mtu kujitoa uhai, Makala ya Afya yako inafafanua hilo. Mtayarishaji ni Amina Abubakar.
Je, unazifahamu dalili za ukomo wa hedhi, kuna hatari yoyote na unawezaje kuzitambua na kushuzishughulikia kwa namna salama?
Je, unazifahamu dalili za ukomo wa hedhi, kuna hatari yoyote na unawezaje kuzitambua na kushuzishughulikia kwa namna salama?
Matumizi ya lugha ya mkato katika mawasiliano
Vijana mchakamchaka leo inaangazia matumizi ya lugha ya mkato katika maisha ya ya kila siku ya kijana.
Kutana na wanawake mabaharia Tanzania
Makala ya wanawake na maendeleo ya DW inajikita zaidi katika kuwaangalia mabaharia wanawake ambao wameamua kufanya kazi hiyo na kuachana na dhana ya kazi hiyo kuwa ya kiume. Ungana na Anuary Mkama kwa mengi zaidi.
Je, ni salama kujamiiana wakati wa ujauzito?
Zifahamu faida za kiafya za kufanya tendo la ndoa wakati wa kipindi cha ujauzito.
Mtindo wa nguo kwa wasioona
Jinsi mtindo wa nukta nundu unavyowasaidia wasioweza kuona
Kurunzi Afya: Tatizo la kukosa usingizi
Kukosa usingizi ni tatizo la kiafya ambalo linawakumba watu wengi, wataalamu wanaeleza baadhi ya sababu zinazochangia hali hiyo, ni kuota ndoto mbaya, msongo wa mawazo na matumizi ya pombe na dawa za kulevya. Zaidi msikilize daktari Msilikale Sengimana kutoka hospitali ya Njiro SAD Arusha.
Mwangaza wa Ulaya: Nchi za EU zaanzisha ukaguzi wa mipakani
Umoja wa Ulaya unakabiliana na ongezeko la wahamiaji. Hilo limesababisha baadhi ya nchi wanachama wa umoja huo kuanzisha upya ukaguzi wa mipakani ndani ya eneo la nchi za Jumuiya hiyo maarufu Schengen, ambalo kwa kawaida hutakiwa kuruhusu usafiri bila ukaguzi wa watu na mali zao. Ungana na Bakari Ubena.
Ruto atetea rikodi ya uongozi wake wa miaka miwili
Rais William Ruto wa Kenya ametetea rikodi yake ya miaka miwili madarakani akisema hakuna serikali ya nchi hiyo iliyowahi kuweka mikakati madhubuti ya kuiendeleza Kenya kuliko ile anayoiongoza. Rashid Chilumba alikaa na kiongozi aliekuwa ziarani mjini Berlin, Ujerumani na kujadiliana naye juu ya rekodi hiyo pamoja na mambo mengine.
Changamoto ya watoto wenye mahitaji maalumu Ghana
Watoto wenye matatizo ya mifumo ya fahamu wakati mwingine huonekana kama "wamelaaniwa" nchini Ghana na kutelekezwa.
Oumilkheir atutembelea baada ya miaka minne alipostaafu
Unamkumbuka Oumilkheir? Najua wafuatiliaji wetu wengi "wanaimiss" sauti yake adhimu enzi hizo akiwa nasi hapa Idhaa ya Kiswahili. Baada ya miaka kadhaa tangu alipostaafu, Bi Oumi, kama hapa tulivyopenda kumuita ametutembelea, na kupata fursa ya kuzungumza na mwenzetu John Juma.
Familia ya kada wa upinzani aliyeuawa Tanzania yateta
Hivi karibuni nchini Tanzania kumekuwa na matukio ya utekaji watu, kujeruhiwa na wakati mwingine kuuawa. Tukio la hivi karibuni linamhusu kada wa upinzani Ali Kibao aliyekutwa amefariki baada ya kutekwa kabla ya umauti. Sudi Mnette amezungumza na mtoto wake na mjane wake bi Amina Kibao kuhusu kifo cha mumewe katika makala ya Kinagaubaga.
Lishe bora katika kuandaa unyonyeshaji bora
Lishe bora ni kitu cha muhimu wakati mama anapokuwa mjamzito ili kujiandaa kwa ajili ya kumnyonyesha mwanae. Kama wengi tujuavyo, kila mama anahamasishwa kumnyonyesha mtoto wake miezisita ya mwanzo ili kupata lishe bora kabisa anayoihitaji katika ukuaji wake. Kuna mengi ambayo yatakunufaisha ukisikiliza makala ya Afya yako.
Mwangaza wa Ulaya:Viongozi wa EU wajadili msaada kwa Ukraine
Mzozo kati ya Urusi na Ukraine ambao unaelekea kuingia katika mwaka wa tatu unazidi kutokota. Mwishoni mwa mwezi Agosti, mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya walijadiliana kuhusu kuongeza msaada wa kijeshi kwa Ukraine. Lakini pia mzozo huo umezusha hali ya hofu kwa mataifa ya Baltic yanayopakana na Urusi ambayo yanahofia kwamba wakati wowote wanaweza pia kushambuliwa. Ungana na Bakari Ubena.
Kukatika kwa mawasiliano baina ya marafiki, tatizo ni nini?
Hali ya kupotezeana imekuwa jambo la kawaida hasa baada ya marafiki kuunganishwa kupitia mitandao ya kijamii.
Wanawake na Maendeleo
Bi. Asawar Mustafa, mwanamke mkimbizi kutoka Sudan anayefanya kazi ya ufundi wa magari nchini Libya amefanikiwa kwa vitendo na kuonesha kwamba mwanamke pia anaweza kuwa fundi gereji hodari na kwamba kazi hiyo si ya wanaume pekee. Makala hii imeandaliwa na Zainab Aziz.
Dhulma dhidi ya waandishi habari Kenya
Katika makala ya Mbiu ya Mnyonge leo, mwandishi wa DW Musa Naviye anaangazia dhulma walizopitia waandishi wakati wa maandamano ya kuipinga serikali nchini Kenya. Baadhi ya waandishi walipigwa risasi na kupitia madhila mengine mikononi mwa maafisa wa polisi wakati walipokuwa wakifanya kazi yao ya kuuhabarisha umma.
Sura ya Ujerumani: Umaarufu wa AfD Ujerumani Mashariki
Makala ya Sura ya Ujerumani inamulika je, ushawishi mkubwa wa chama cha AfD mashariki mwa Ujerumani unatokana na nini?
Kutoka London hadi Lagos peke yake kwa gari
Fikiria, alilala na kula wapi? Vipi kuhusu usalama wake? Kutana na msichana Pelumi mzaliwa wa Lagos, Nigeria aliyekulia London Uingereza. Alitaka kuvunja rekodi ya ulimwengu kwa kuwa mwanamke wa kwanza aliyesafiri mwenyewe kati ya mabara mawili ya Ulaya na Afrika. Tizama safari yake ya kutoka London hadi Lagos akiendesha mwenyewe gari dogo. #Vijanamubashara
Je, Polisi wapewe mafunzo maalumu kukabili maandamano?
Wakati wa maandamano maafisa polisi hushuhudiwa wakitumia nguvu kupita kiasi. Katika vidio hii Mtaalamu wa usalama wa Kenya Byron Adera anachambua jinsi polisi wanapaswa kuyadhibiti maandamano. #vijanamubashara
Mji wangu - Soweto
Kitongoji cha Soweto kinapatikana viungani mwa jiji la Johannesburg. Kimekuwa jukwaa la baadhi ya matukio muhimu katika historia ya Afrika Kusini. Mmoja wa wasanii maarufu wa mitaani mjini humo, Senzo Nhlapo, anatutembeza katika kitongoji hiki chenye uchangamfu.
Wanawake na Maendeleo: Jeniffer Shigoli mtetezi wa haki za wanawake na mabinti
Jeniffer Richard Shigoli ni mwanaharakati anaesimamia masuala ya usawa wa kijinsia kupitia kampeni yake ya 'Binti Huru' anawasaidia watoto wa kike walio shuleni waweze kuepukana na vikwazo vitokanavyo na hedhi sabamba na kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wanawake walio katika mazingira duni ili waweze kuepukana na umasikini.
Je unasoma masharti wakati wa manunuzi mtandaoni
Sema Uvume je umeshakutana na masharti na makubaliano ama kwa kimobo Terms and Agreements wakati unaponunua vitu mitandaoni? Je, unayasoma na kuyaelewa masharti hayo? Athari za kutoyasoma ni zipi? Sema Uvume inakupa majibu mtayarishaji ni Suleman Mwiru.
Ipi sababu ya kijana kusoma vitabu vya hadithi kuliko dini?
Katika kipindi cha Vijana Mubashara, Jacob Safari anauliza je unafikiri ni kwanini vijana wako radhi kusoma vitabu vya hadithi au riwaya kuliko vitabu vya kidini?
Msimamo wa serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar
Ikiwa ni mwaka mmoja kabla ya uchaguzi kufanyika mwakani, mwandishi wetu wa Zanzibar Salma Said, amezungumza na Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, kujua je juhudi gani ambazo wamezifanya kuinusuru serikali ya umoja wa kitaifa kabla kuporomoka?
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 1 wa 5
Ukurasa unaofuatia