Maelfu ya watu wahamishwa Italia kufuatia Kimbunga Boris
19 Septemba 2024Matangazo
Naibu Waziri wa Uchukuzi Galeazzo Bignami amewaambia waandishi wa habari kwamba watu wawili haijulikani walipo. Shule zilifungwa na huduma za treni zimesitishwa kwa muda. Upepo mkali na mvua kubwa vimeshuhudiwa Ulaya ya kati na mashariki na kuua takriban watu 24. Kimbunga Boris kimasababisha mafuriko na kuyaathiri mataifa ya Austria, Jamhuri ya Czech, Poland na Romania. Wataalamu wanasema mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababishwa na utoaji wa gesi chafuzi inayotokana na shughuli za binadamu, yanaongeza kasi ya majanga hayo ya asili.