Kongo: Mapigano yapamba moto kati ya jeshi na waasi wa M23
8 Novemba 2023Vyanzo vya kiraia pia katika eneo hilo, vimeeleza kuwa asubuhi ya leo kikosi cha jeshi la Burundi kiliteketeza moto baadhi ya vifaa vyake kwenye kambi yao ya mjini Kitshanga kabla kikosi hicho kuelekea katika sehemu isio fahamika.
Tangu alfajiri mapema kwenye ngome ya jeshi tiifu kwa serikali katikati mwa mji wa Kilolirwe ulio karibu kilometa 30 kutoka sake wilayani masisi.
Katika tangazo lao kwenye mtandao wa X , kundi hilo lilitangaza kuudhibiti mji huo unaounganisha eneo hilo na Goma baada yakuteka pia milima ya Gicwe iliyokuwa ngome muhimu ya jeshi la Congo nakuendelea hadi mji mdogo wa Kausa.
Hadi jioni leo, mamia wa raia wanaokimbia wamiminika katika mji wa sake, kimometa 25 kutoka Goma.
Soma pia:Blinken azungumza na Kagame na Tshisekedi kuhusu M23
Wakati hayo yakiendelea, kikosi cha jeshi kutoka nchini Burundi kilichopelekwa kwenye eneo hilo ili kuleta utulivu, kimeteketeza kwa moto baadhi ya vifaa vyake ikiwemo zana za kivita katika kambi yao mjini Kitshanga.
Kulingana na vyanzo vya kiraia kumeongeza wasiwasi baada ya kikosi hicho kuondoka na kuelekea sehemu isiyofahamika.
Pande za mzozo zatupiana lawama
Waasi wa M23 kwa siku kadhaa, wamekuwa wakiwashutumu wanajeshi wa Burundi kwa kushirikiana na askari wa Kongo katika mapigano hayo yanayoendelea kusambaa.
Tuhuma hizo zilikanushwa na serikali ya Burundi miezi michache iliyopita.
Hali hiyo ya wasiwsi pia ,ilishuhudiwa katika miji ya Buhumba na kibati wilayani Nyiragongo ambako ndege za kivita zilitumiwa na jeshi la Kongo kwa kuzibomoa kwa mizinga ngome za waasi wa M23.
Soma pia:Mapigano yaendelea mji wa Kitshanga Kongo
Mapigano yamesababaisha uharibifu mwingine wa waya zinazo sambaza umeme katika mji wa Goma siku moja baada waya hizo kufanyiwa marekebisho.
Sehemu kubwa ya mji wa Goma unaokaliwa na zaidi ya watu milioni moja imegubikwa na giza ambalo madhara yake yatakuwa mabaya zaidi.