1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Congo lawazuia waasi wa M23 kuingia Goma

7 Novemba 2023

Jeshi la Congo FARDC Jumatatu lilizima jaribio jipya la waasi wa M23 kuingia mji wa Goma. Vyanzo vya kijeshi vimeeleza kuwa waasi hao walirudi nyuma baada ya masaa kadhaa ya mapigano katika eneo la Kibati na Buhumba.

https://p.dw.com/p/4YV3E
Wanajeshi wa Kongo Butembo | wakiimarisha ulinzi
Wanajeshi wa FARDC Picha: JOHN WESSELS/AFP/Getty Images

Wakati huo huo kikosi cha Umoja wa Mataifa kimeanzisha rasmi operesheni ya "Springbok" baada ya kuweka kambi yao katika mji mdogo wa Kimoka  wilayani Masisi ili kuzuia kusonga mbele kwa M23.

Vyanzo vya kijeshi vimeeleza kuwa waasi hao wa M23 wanaodaiwa kusaidiwa na jeshi la Rwanda walijaribu kujipenyeza kwenye ngome kuu ya wanajeshi tiifu kwa serikali ya Congo kwenye milima ya kanyamahoro wilayani Nyiragongo ambako walilenga kwa makombora.

Umeme wakatika mji wa Goma

Hata hivyo, katika mapigano hayo yaliyodumu kwa masaa kadhaa, jeshi la Congo linalosaidiwa na makundi ya wapiganajii wazalendo walifaulu kuzima jaribio hilo kwa kurusha mizinga kuelekea ngome za M23 kwenye bonde la Buhumba na Kibati.

Wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo
Wakaazi waondoka vijiji vya Kibati na Kibumba baada ya vita kati ya FARDC na M23 24.05.2022Picha: ESDRAS TSONGO/AFP via Getty Images

Athari za mapigano hayo ni chungunzima ikiwemo uharibifu wa nyaya zinazosambaza umeme katika mji wa Goma ambao ulitumbukia katika giza huku raia wanahangaika kutokana na ukosefu wa huduma hiyo.

Wakati huo huo, kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Congo, MONUSCO pamoja na maafisa wa jeshi la Congo, wamezindua operesheni ya SpringBok kwenye milima ya Kimoka ambayo lengo ni kuzuiya kusonga mbele kwa  waasi wa  M23 na kuiteka miiji ya Sake na Goma.

MONUSCO yashindwa kuumaliza mzozo wa Congo

Mazungumzo hayo mbele ya vyombo vya habari ,yalifuatiwa na mazoezi ya kijeshi ndani ya kambi hiyo iliyopo katika eneo la Kimoka, karibu kilometa 2 kutoka mji wa kimkakati wa Sake kwenye barababara inayoelekea Kilolirwe na Kitshanga Masisi maeneo yananayokaliwa na waasi wa M23 .

Kongo I Mkutano kati ya M23 na kikosi cha kulinda amani cha Afrika Mashariki
Mwakilishi wa M23 Kanali John Imani NzenzePicha: Guerchom Ndebo/AFP

Kwa miaka kadhaa sasa, suala la kuondoka kwa vikosi vya MONUSCO nchini Congo limekuwa chanzo cha mvutano kati ya miungano ya kiraia na ujumbe huo unaotuhumiwa kushindwa kumaliza mzozo mashariki mwa taifa hilo, eneo linaloyumbishwa na vita kati ya makundi ya waasi na jeshi la Congo kwa zaidi ya miongo miwili.