Italia yatangaza hali ya hatari kufuatia mafuriko
21 Septemba 2024Italia imetangaza hali ya hatari leo Jumamosi kufuatia mafuriko makubwa katika mikoa yake miwili ya Emilia-Romagna na Marche iliyopo kazkazini mwa nchi hiyo. Hali hiyo imetangazwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Giorgia Meloni na kusema kwamba dola milioni 22 zinahitajika haraka kama msaada wa dharura.
Mvua kubwa imesababisha barabara nyingi kujaa maji katika mikoa hiyo miwili, zaidi ya watu 2,500 wamelazimika kuyakimbia makaazi yao. Miji ya pwani ya Bologna, Modena na Ravenna ni miongoni mwa miji iliyokubwa na kadhia hiyo.
Soma zaidi. Maelfu ya watu wahamishwa Italia kufuatia Kimbunga Boris
Wakati huo huo, kumekuwepo na kutupiana maneno ya lawama kati ya serikali mjini Roma na
serikali za mikoa ya maeneo yaliyokumbwa na mafuriko. Nello Musumeci,Waziri wa ulinzi kutoka serikali hiyo ya mrengo wa kulia alimshutumu kiongozi wa mji wa Emilia-Romagna kutoka chama cha social-demokratic kwa kutotumia pesa ambazo tayari zilikwishatolewa kwenye mji huo.
Kwa upande wao Social-Democrats walizijibu tuhuma za waziri huyu na kusema kwamba hizo ni njama kuelekea uchaguzi katika jimbo hilo utakaofanyika hapo mwezi Novemba.