Waliozama katika jahazi la kifahari Italia, bado wapo hai
21 Agosti 2024Matangazo
Ripoti zinaarifu kwamba walinzi wa pwani ya Italia bado hawajauondoa uwezekano kwamba watu wasiojulikana walipo kufuatia ajali hiyo, akiwemo bilionea wa Uingereza Mike Lynch na mwanawe wa kike Hannah, aliye na umri wa miaka 18, bado wako hai. Baada ya ajali hiyo, mwili mmoja ulipatikana katika eneo la tukio mtu huyo akitambulishwakama mfanyakazi aliyekuwa katika jahazi hilo, ambaye uraia wake ni wa Canada. Shirika la zima moto la Italia linasema kwamba kwa sasa linachora mkakati wa kuingia katika jahazi hilo ambalo liko mita 50 chini ya bahari. Operesheni hiyo ya uokozi imeendelea kwa zaidi ya masaa 36 sasa.