1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Geneva:Chama cha mrengo wa kulia chatarajiwa kurudi madarakani Uswisi.

21 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Dq

Vituo vya kupigia kura vimefungwa nchini Uswisi kukisubiriwa matokeo ya uchaguzi wa bunge. Kura za maoni ya wapiga kura zinaashiria chama cha mrengo wa kulia People´s Party kitarudishwa madarakani. Chama hicho kimeendesha kampeni yenye mabishano kikitoa wito wa kurejeshwa makwao wageni wanaotenda makosa makubwa ya uhalifu. Kampeni yake iliokosolewa vikali ni pamoja na mabango yenye picha ya nguruwe watatu weupe wakimfukuza nchini nguruwe mweusi. Wapinzani wa chama hicho wanasema hali hiyo inaweza kuhujumu sura ya Uswisi nchi za nje.