1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GÖTTINGEN: Chama cha Kijani kinapinga ujumbe wa Tornado

16 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBPL

Wajumbe katika mkutano maalum wa chama cha Kijani cha Ujerumani kwa wingi mkubwa wamepiga kura kupinga kurefusha ujumbe wa Ujerumani nchini Afghanistan.Kura 361 zimepinga na 264 zimeunga mkono.

Ujumbe wa ndege za upelelezi aina ya Tornado, umekosolewa vikali na umepingwa kabisa. Ujumbe wa pili wa Ujerumani nchini Afghanistan, unahusika na vikosi vinavyoshirikiana na majeshi ya kimataifa kulinda usalama ISAF.Kwa mujibu wa chama cha Kijani ujumbe huo unaweza kuendelea kwa masharti makali.

Wabunge 51 wa chama cha Kijani,wameshauriwa kupinga tume zote mbili,kura zitakapopigwa bungeni mjini Berlin,katika mwezi wa Oktoba.