UNICEF: Mtoto 1 kati ya 4 anakabiliwa na ukosefu wa chakula
6 Juni 2024Matangazo
Kulingana na UNICEF, idadi hiyo inamaanisha kwamba zaidi ya watoto milioni 180 wanakabiliwa na kitisho cha kuathirika katika ukuaji.
Mkuu wa UNICEF Catherine Russell amesema watoto wanaokula makundi mawili tu ya chakula kwa siku kama wali na maziwa wana uwezekano wa zaidi ya asilimia 50 wa kupata aina mojawapo ya utapiamlo mkali.
Umaskini mkubwa wa chakula kwa watoto umekithiri katika nchi kama 20, na hasa Somalia, ambapo asilimia 63 ya watoto wadogo wameathirika; Guinea, Guinea-Bissau na Afghanistan.