Watoto 700,000 hatarini kupata utapiamlo hatarini - UNICEF
9 Februari 2024Msemaji wa UNICEF, James Elder, alisema bila ya kupata msaada wa ziada shirika hilo halitaweza kuwatibu zaidi ya watoto 300,000 kati ya wale wasiofikiwa vyema, na kwa hivyo makumi ya maelfu huenda wakafa.
Soma zaidi: UNICEF yaomba dola bilioni 9.3 za kusaidia watoto 2024
Elder aliainisha aina mbaya zaidi ya utapiamlo, ambao unamfanya mtoto awe na uwezekano mara kumi wa kufa kutokana na maradhi kama vile kipindupindu na malaria.
Soma zaidi: Mataifa zaidi kuwaondoa raia wao Sudan
Alisema watoto milioni 3.5 wanatazamiwa kukumbwa na utapaiamlo huo mbaya.
Siku ya Alhamis (Februari 8), Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, aliayahimiza mataifa kutowasahau raia waliozingirwa katika vita vya Sudan, na kutoa maombi ya dola bilioni 4.1 ili kushughulikia mahitaji yao ya kiutu.