1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Usalama wa chakulaSomalia

WFP: Somalia itakabiliwa na njaa kali kufuatia mafuriko

15 Novemba 2023

Shirika la chakula duniani WFP limesema robo tatu ya idadi ya watu wa Somalia, wapo hatarini kukabiliwa na njaa kali zaidi mwaka huu kutokana na hali ya ukame na mafuriko yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

https://p.dw.com/p/4YpQ1
Mkazi wa Mogadishu akipita katikati ya mafuriko kufuatia mvua kubwa zinazonyesha Somalia
Mkazi wa Mogadishu akipita katikati ya mafuriko kufuatia mvua kubwa zinazonyesha SomaliaPicha: Feisal Omar/REUTERS

Mapema mwaka huu Umoja wa Mataifa ulieleza kuwa mafuriko ambayo yalisababisha maelfu ya watu nchini Somalia na katika nchi jirani za Afrika Mashariki kuyahama makazi yao ni mojawapo ya matukio matukio makubwa ya karne.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani limesema mafuriko hayo yameathiri jamii ambazo tayari zinapambana kujikwamua kutokana na ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika miongo minne uliosababisha mamilioni ya watu kukabiliwa na njaa.

Soma zaidi: Mafuriko yauwa 29 wengine maelfu wayahama makaazi yao

Wafanyabiashara na wakaazi katika mji huo wa Dolow wamesema, athari ni kubwa kwa kuwa hakuna bidhaa zinazoingia na maisha yao watu yapo hatarini.

Kw mjibu wa mwanamke mmoja alielazimika kuyahama makazi yake amesema alilazimika kutoka kijiji cha Galbolow baada ya nyumba na vibanda kujaa maji. Hakuna huduma za kijamii vyakula na magodoro yalisombwa na maji, na kuna uhaba mkubwa wa bidhaa ikiwemo chakula na mafuta."

Bi. Fatima Abdi muhanga wa mafuriko nchini Somalia
Bi. Fatima Abdi muhanga wa mafuriko nchini SomaliaPicha: Feisal Omar/REUTERS

Wakaazi wa mji huo pia wamesema wanashindwa kwenda kwenye baadhi ya maeneo ya miji na vijiji kwa sababu ya maji yaliyofurika lakini pia wanahofia usalama wao huenda wakadhuriwa na wanyama wakali wa majini wanaokuja na mafuriko wakiwemo mamba. 

Msemaji wa shirika la WFP nchini Somalia Petroc Wilton, amesema maisha ya watu takribani milioni 4.3 yatakuwamo hatarini kufikia mwishoni mwa mwaka huu. Ametoa wito kwa jumuiya za kimataifa kutoa msaada.

WFP Imetoa wito kwa jumuiya za kimataifa kuongeza msaada

Kwa upande wao Shirika la Misaada la World Vision kupitia meneja wao wa oparesheni nchini humo Muhidin Abdullahi amesema wao wameokoa zaidi ya watu 400 kutoka maeneo yaliyozama kabisa kwenye maji kufuatia mvua kubwa iliyonyesha wiki iliyopita. Pia wameokoa baadhi ya wanakijiji waliokuwa wamekwama kutokana na mafuriko.

Soma zaidi: EU yasitisha kwa muda ufadhili Somalia

Mabadiliko ya hali ya hewa yaliyoleta ukame yalichangia pakubwa vifo vya mamilioni ya mifugo na kuharibu hekta zisizohesabika za mashamba na maeneo ya malisho. Mafuriko yameizima kabisa ahueni na kusababisha majanga nchini humo. Baadhi ya familia kutoka Dolow zimehamishiwa katika kambi za wakimbizi wa ndani.