1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaIndia

Wokoaji wanapambana kufikia wahanga wa mafuriko India

Hawa Bihoga
7 Oktoba 2023

Vikosi vya uokoaji nchini India vimeripoti kupata changamoto kufikia maeneo yaliokumbwa na mafuriko katika jimbo la Kaskazini mashariki la Sikkim, ambako zaidi ya watu 140 hawajulikani walipo.

https://p.dw.com/p/4XEuY
Waokoaji wa mafuriko India wakijaribu kutumia vifaa mbadala kuwafikia wahanga zaidi
Waokoaji wa mafuriko India wakijaribu kutumia vifaa mbadala kuwafikia wahanga zaidiPicha: Prakash Adhikari/AP Photo/picture alliance

Katibu Mkuu wa jimbo hilo V.B.Pathak amesema, kinachosubiriwa ni kuboreka kwa hali ya hewa ili kikosi cha anga na timu zingine za uokoaji zijitose katika maeneo yaliokumbwa na mkasa huo ili kutafuta wahanga.

Soma pia:UNICEF: Majanga yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa yalisababisha watoto milioni 43.1 kupoteza makazi yao kati ya mwaka 2016 hadi 2021

Hadi sasa idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko hayo,imiongezeka hadi kufikia 44 kutoka watu wawili siku ya Ijumaa, kulingana na mamlaka ya mji mkuu wa jimbo hilo Gangtok.

Kingo za Ziwa la Lhonak zilipasuka siku ya Jumatano baada ya mafuriko yaliyosababishwa mvua kubwa na maporomoko ya theluji, na kusababisha mafuriko makubwa katika mto Teesta.