1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sergio aongoza duru ya kwanza ya uchaguzi Argentina

23 Oktoba 2023

Waziri wa masuala ya uchumi wa Argentina, Sergio Massa, ameshinda katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais na sasa atapambana na mshindi wa pili, Javier Milei, katika duru ya pili hapo Novemba 19.

https://p.dw.com/p/4XtvU
Waziri wa Uchumi Argentina Sergio Massa
Waziri wa Uchumi Argentina Sergio MassaPicha: Natacha Pisarenko/AP Photo/picture alliance

Waziri huyo wa uchumi kutoka muungano wa mrengo wa kushoto wa Union for the Homeland alipata karibu asilimia 36 ya kura, hii ikiwa ni kulingana ofisi ya uchaguzi Jumapili usiku, wakati kura karibu zote zikiwa zimehesabiwa.

Javier Milei wa chama cha Freedom Advances aliyepigiwa upatu kwa kiasi kikubwa alishika nafasi ya pili kwa asilimia 30. 

Soma pia:Argentina kuandaa duru ya pili ya uchaguzi wa rais

Waziri wa zamani wa mambo ya ndani Patricia Bullrich kutoka muungano wa upinzani wa kihafidhina wa Together for Change ulishika nafasi ya tatu kwa kupata chini ya asilimia 24.