1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi 6 kuwa wenyeji wa Michuano ya Kombe la Dunia 2030

5 Oktoba 2023

Shirikisho la Soka Ulimwenguni FIFA, limefahamisha hapo jana kuwa michuano ya Kombe la Dunia la wanaume mwaka 2030, itaandaliwa katika nchi sita na mabara matatu.

https://p.dw.com/p/4X7mV
Symbolbild | World Cup 2030 - WM Trophäe
Picha: Mike Egerton/empics/picture alliance

Nchi hizo ni Uhispania, Ureno, Morocco, Uruguay, Argentina na Paraguay.

Katika taarifa yake, FIFA imesema mechi zitakazochezwa Amerika Kusini, itakuwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 100 ya Kombe la kwanza la Dunia nchini Uruguay. Morocco itakuwa taifa la kwanza la Afrika Kaskazini kuwa mwenyeji wa michuano hiyo.

Hata hivyo makubaliano hayo ya FIFA kuhusu  Kombe la Dunia  la mwaka 2030 yanapaswa kuidhinishwa na mashirikisho 211 wanachama yatakayo jumuika katika kikao hapo mwakani. Marekani, Mexico na Canada ndiyo watakaokuwa wenyeji wa Kombe la Dunia la mwaka 2026.