SiasaIraq
Iraq kuanza kuondoa majeshi ya muungano
6 Januari 2024Matangazo
Hatua hiyo inafikiwa siku moja baada ya shambulizi la Marekani lililomuua kamanda wa wanamgambo wanaoiunga mkono Iran.
Ofisi ya Waziri Mkuu Mohamed al-Sudan imesema serikali inapanga tarehe ya kuunda kamati ya pamoja itakayoweka mipango ya kuviondoa moja kwa moja vikosi hivyo nchini Iraq.
Kuna wanajeshi karibu 2,500 nchini Iraq, pamoja na 900 kutoka Syria, ambao ni sehemu ya juhudi za kulizuia kundi linalojiita Dola la Kiislamu, kujiimarisha.
Uamuzi wa Al Sudani unachukuliwa wakati upande wa wabunge unaoiunga mkono Iran na unaomuunga mkono waziri mkuu wakilaani vikali mauaji ya kamanda huyo Mustaq Jawad Kazim al Jawari mjini Baghdad, siku ya Alhamisi.