1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Ugaidi

Watu 11 wauawa katika shambulio la bomu Iraq

1 Desemba 2023

Watu 11 wameuawa mashariki mwa Iraq katika shambulio lililofanywa na watu waliojihami kwa silaha ambalo linadaiwa kufanywa na wapiganaji wa jihadi.

https://p.dw.com/p/4ZecJ
Baghadad, Iraq| Mashambulizi ya kujotoa muhanga
Vikosi vya usalama vimelaumu kundi la wapiganaji wa jihadi kuhusika na mashmabulizi.Picha: Hadi Mizban/AP/picture alliance

Watu 11 wameuawa mashariki mwa Iraq katika shambulio lililofanywa na watu waliojihami kwa silaha ambalo

Bomu lililotegwa kando kando mwa barabara liliripuka huku watu waliokuwa na silaha wakifyatua risasi kiholela.

Gavana wa mkoa wa Diyala, ulioko nje kidogo ya mji mkuu Badhdad, Muthana al-Tamimi ameshtumu vikali shambulio hilo kwa kile alichokiita "shambulio la uwoga lililofanywa na kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS."

Soma pia: Irak yalaani mashambulizi ya angani ya Marekani Baghdad

Katika ukurusa wake wa kijamii wa Facebook, gavana huyo amehimiza vikosi vyake vya usalama kuwa macho dhidi ya oparesheni za makundi ya kigaidi.

IS hata hivyo haikudai mara moja kuhusika na shambulio hilo japo ina seli kadhaa katika mkoa wa Diyala.