Irak yalaani mashambulizi ya angani ya Marekani Baghdad
22 Novemba 2023Katika taarifa, kundi hilo lililojihami limesema mashambulizi hayo yamewauwa hao wanachama wake katika ngome yake ya Jurf al-Sakhar. Kataib Hezbollah limetishia kufanya mashambulizi zaidi iwapo Marekani itaendelea kushambulia.
Marekani imefanya msururu wa mashambulizimawili Iraq tangu jana na hiyo kutokana na zaidi ya mashambulizi 60 yaliyofanywa na wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran dhidi ya majeshi katika eneo hilo.
Soma pia:Marekani imesema tayari imeshambuliwa karibu mara 66 na wanamgambo nchini Iraq
Hadi wiki hii, Marekani ilikuwa haijafanya uamuzi wa kulipiza kisasi nchini Iraq kwasababu ya hali tete ya kisiasa nchini humo, ambapo marekani inatafuta ushirikiano wa karibu na pia ilikuwa haitaki ionekane kana kwamba ni kutanuka kwa vita vya Israel dhidi ya hamas katika eneo hilo la Mashariki ya Kati.