Wanajeshi 2 wa Iraq na wapiganaji 2 wa Peshmerga wauliuwa
23 Oktoba 2023Wanajeshi wawili wa Iraq na wapiganaji wawili wa vikosi vya kikurdi vya Peshmerga wameuliwa jana Jumapili wakati pande hizo mbili zilipokabiliana kwenye eneo la milima la kaskazini mwa Iraq. Hayo ni kwa mujibu wa duru za usalama za Iraq na Kurdistan.
Waziri Mkuu wa Iraq na amiri jeshi mkuu Mohammed Shia al-Sudani ameamuru kuundwe kamati maalum kuchunguza mapigano hayo. Duru hizo zimesema wapiganaji wa chama cha wafanyakazi wa Kikurdi, Kurdistan Workers Party PKK walikuwa wameondoka kutoka maeneo waliyokuwa wakiyadhibiti karibu na mji wa Makhmour siku ya Jumamosi na kuyakabidhi kwa jeshi la Iraq.
Lakini wapiganaji wa Pershmerga wa chama cha Kurdistan Democratic, KDP, chama tawala cha eneo lenye utawala wake wa ndani la Kurdistan, wakajaribu kuyachukua tena maeneo hayo jana Jumapili, na hivyo kuzua mapigano.