1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu wa Haiti afanya ziara nchini Marekani

2 Julai 2024

Waziri mkuu mpya wa Haiti Garry Conille amesema Marekani imejitolea zaidi katika kusaidia kikosi cha kimataifa, kinachoongozwa na Kenya kilichotumwa nchini humo ili kukomesha ghasia za magenge ya kihalifu.

https://p.dw.com/p/4hl0l
Waziri mkuu mpya wa Haiti Garry Conille
Waziri mkuu mpya wa Haiti Garry Conille Picha: Guerinault Louis/Anadolu/picture alliance

Waziri mkuu mpya wa Haiti Garry Conille amesema Marekani imejitolea zaidi katika kusaidia kikosi cha kimataifa, kinachoongozwa na Kenya kilichotumwa nchini humo ili kukomesha ghasia za magenge ya kihalifu.

Conille ambaye aliapishwa mwezi uliopita kama waziri mkuu wa serikali ya mpito katika taifa hilo lililokumbwa na mgogoro, anafanya ziara mjini Washington na anatazamiKikosi cha polisi wa Kenya kuelekea Haiti Juni 25wa kukutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken na mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa Kristalina Georgieva leo Jumanne. Kikosi cha polisi wa Kenya kuelekea Haiti Juni 25

Nchi kadhaa, nyingi za Afrika na Karibiani, zinatarajiwa kushiriki katika misheni hiyo, ambayo inaungwa mkono na Umoja wa Mataifa. Rais Joe Biden amekataa kutuma wanajeshi wa Marekani nchini Haiti, lakini amesema nchi hiyo itatoa ufadhili kwa kikosi cha kimataifa chenye jukumu la kusaidia polisi kukomesha magenge ya wahalifu yaliyo na nguvu.