JangaAsia
Watu 48 wafariki baada ya barabara kuporomoka China
2 Mei 2024Matangazo
Hayo ikiwa ni kulingana na vyombo vya habari vya serikali ambavyo vimeeleza pia kuwa juhudi za uokoaji zinaendelea.
Hapo jana, sehemu ya barabara inayotoka katika jiji la Meizhou kuelekea kaunti ya Dabu iliporomoka kutokana na mvua kubwa zilizonyesha eneo hilo, jambo lililopelekea magari kadhaa kuanguka kwenye korongo la karibu mita 18.
Soma pia:Iran na China zatia saini makubaliano ya ushirikiano
Katika wiki za hivi karibuni, mji wa viwanda na wenye watu wengi wa Guangdong, umekuwa ukikumbwa na msururu wa majanga yatokanayo na hali mbaya ya hewa ikiwa ni pamoja na dhoruba.
China hutoa idadi kubwa ya gesi chafuzi kwa mazingira lakini imeahidi kupunguza maradufu uzalishaji huo ifikapo mwaka 2060.